Mkurugenzi
wa Masoko na Utafiti, Raphael Mwamoto akitoa maelezo ya huduma
zinazotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa Naibu Waziri wa
Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi wakati alipotembea banda la
Mfuko katika maonesho ya Nane Nane mkoani Lindi.
Meneja wa Mkoa wa Lindi, Fortunata Raymond akielezea namna Mfuko wa Afya ya Jamii unavyofanya kazi Mkoani humo.
Naibu
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi akisisitiza jambo
baada ya kupata maelezo ya huduma za Mfuko huo ikiwa pamoja na
kuupongeza kwa kazi nzuri.
Ofisa
Mdhibiti Ubora wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Timothy Mwasajone
akitoa ushauri wa namna ya kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza.
SERIKALI imeutaka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuendesha
huduma za elimu ya kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza katika mikoa
yote hususani vijijini pamoja na upimaji wa afya bure ili wananchi
watambue afya zao na hatimaye kuongeza uzalishaji katika sekta za kilimo
na uvuvi na biashara kwa ujumla.
Agizo hilo lilitolewa na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na
Ushirika Godfrey Zambi wakati wa maonesho ya Nane Nane Kitaifa
yanayoendelea mkoani Lindi ambapo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
umeshiriki na unatoa huduma mbalimbali zikiwemo za elimu kwa Umma,
usajili wa wanachama, upimaji afya bure ikiwemo saratani ya matiti.
Aidha alisisitiza kuwa mbali na huduma hizo nzuri zinazotolewa
na Mfuko, ni vyema wananchi pia wakapata elimu juu ya umuhimu wa
kujiunga na Mifuko ya Afya ya Jamii ili wanapougua wapate matibabu bila
ya usumbufu wowote.
“NHIF mnafanya kazi nzuri sana nawapongeza, na hata huduma
mliyoileta huku Lindi katika kipindi hiki cha siku nane naamini wananchi
wa maeneo haya watanufaika na huduma hizi hususan ya upimaji wa afya
bure, hivyo ninachowaomba sasa ongezeni kasi hasa kwa kwenda vijijini
ambako ndiko kuna kundi kubwa la wananchi,”
“Wakati mkifanya hizi huduma pia wahamasisheni wananchi kujiunga
na Mifuko hii ya Afya ya Jamii ili wanapougua wapate huduma hata kama
hawana fedha mfukoni,” alisema Naibu Waziri.
Aidha alitoa mwito kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi, Mtwara na
wananchi wanaoishi jirani na mikoa hiyo kuhakikisha wanaitumia vyema
fursa hii wakati wa maonesho haya kufika katika banda la NHIF ili kupata
huduma ambazo zinatolewa bila malipo kwa wananchi lakini zimeghramiwa
na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Naye Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Raphael Mwamoto, alisema
kuwa NHIF kwa sasa inaendesha huduma hizi katika mikoa yote kwa lengo la
kuwafanya wananchi kutambua umuhimu wa kujua afya zao lakini pia
umuhimu wa kupata huduma za matibabu kupitia Mifuko ya Afya ya Jamii.
Alisema kuwa kwa upande wa elimu juu ya faida za kujiunga na
Mifuko ya Jamii, NHIF inao mpango wa elimu ya Kata kwa Kata ambayo
inafanyika zaidi katika maeneo ya vijijini ili kuwahamasisha wananchi
kujiunga na kunufaika na Mifuko hii.
“Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa sasa una ofisi zake kila
Mkoa Tanzania ikiwemo Ofisi ya Zanzibar, hivyo shughuli za elimu kwa
umma na upimaji wa afya za wananchi hufanywa mara kwa mara na maofisa wa
Mfuko walioko katika Ofisi zetu za mikoani” alisema.
Pia Ndugu Mwamoto aliendelea kusema kwamba matumizi sahihi ya
fedha za tele kwa tele za CHF pamoja na fedha za matibabu zinazolipwa
na NHIF katika vituo vinavyotoa huduma kwa wanufaika wa CHF na NHIF ni
jambo muhimu sana. Alisema……..….’’ Fedha zinazolipwa na Mfuko pamoja na
CHF ni fedha nyingi ambazo zikitumika vizuri zinaweza kuboresha huduma
za afya hasa upatikanaji wa dawa maeneo ya vijijini, kuna Halmashauri
ambazo zimefanikiwa sana katika hili kwa mfano Nachingwea, Iramba,
Igunga. Zingine ni Halamsahauri za Songea,Tanga ,Rombo,Singida na
Mwanga. Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unaziomba Halmashaouri zingine
nchini kote ziige mfano huu’’,
0 comments:
Post a Comment