Wanannchi
wa mikoa ambayo haijafikiwa na awamu ya tatu ya mradi wa mfuko wa
maendeleo ya jamii nchini TASAF wametakiwa wajiandae kupata maendeleo
kwani mradi huo utawafikia kwa ajili ya kuzitambua kaya masikini na
kiziandikisha kwa ajili ya kupeleka miradi ya maendeleo.
Akizungumza
katika mahojiano maalumu na mtandao huu mkurugenzi mtendaji wa mfuko huu ndg Ladislaus Mwamanga (pichani )
amesema kwenye awamu ya tatu ya TASAF tayari mikoa ya Lindi na Mtwara
imekwishafikiwa kwenye sekta ya afya, elimu na lishe bora na sasa
wananchi wanafurahia maendeleo kutokana na mfuko huu kutoa fedha katika
awamu nne za utekelezaji kwa miezi ya ,January, March, May na July.
Ndg
Mwamanga Ameongeza kusema kuwa sasa TASAF inaendelea kuzifikia wilaya 19
za mikoa ya Dodoma, Singida na katavi kuzitambua na kuziandikisha kaya
masikini.
ndg
Mwamanga amesema kasi ya mafanikio inatokana na elimu wanayoitoa kwa
viongozi wa halmashauri kwa ajili ya kuwaelimisha wananchi juu ya
utekelezaji wa awamu ya tatu ya TASAF na hivyo kuwapongeza viongozi hao
kwa ushirikiano wanaoutoa lengo likiwa ni kiwaletea maendeleo wananchi
ambao ni mpango mama wa serikali.
" TASAF
nado inaendelea na kasi ya kuwajengea uwezo wataalamu wa halmashauri kwa
ajili ya kusambaza elimu katika wilaya nyingine hapa nchini" ambapo
hadi sasa wataalamu hao wamefikia 2500 lengo likiwa ni kufikia wataalamu
4500.
Hata
hivyo mkurugenzi huyo ameendelea kusema kuwa katika,mzunguko wa tatu wa
TASAF halmashauri 160 zitakuwa zimekwisha fikiwa hadi kufikia mwishoni
mwa mwaka huu.
Katika
kipindi cha miaka kumi na mitatu ya utekelezaji wa mipango ya TASAF
miradi mbalimbali ya maendeleo imewafikia wananchini kwenye sekta za
afya, elimu, maji, miundombinu na barabara.
Awamu ya
tatu ya utekelezaji wa mfuko wa maendeleo ya jamii nchini TASAF
ilizinduliwa na rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk Jakaya
Kikwete mwezi wa nane mwaka 2012 mjini Dodoma lengo likiwa ni kuzifikia
kaya masikini nchini kwa kuzitambua na kuziandikisha kwa ajili ya
kuziletea maendeleo na kuondokana na lindi la umasikini nchini.
0 comments:
Post a Comment