Wednesday, 27 August 2014


Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo Msekhela
--------------------------------------------------
Jeshi la polisi mkoani ruvuma liwashikilia askari wake wawili kwa kosa la kumjeruhi dereva pikipiki wenye umri wa mika (22) aliyetambulika kwa jina la salgo ndunguru mkazi wa mtaa wa ruvuma manispaa ya songea mkoani ruvuma .

Kamanda wa jeshi hilo la polisi mkoa wa Ruvuma mihayo msikhela akizungumza na mtandao huu amewataja  askari  ambao wanaoshikiliwa jeshi hilo kuwa ni askari no.G5075 PC WAZAIRI na askari no G9800 PC AYOUB wakiwa katika doria na pikipiki ya polisi yenye namba za usajiri CR aina ya YAMAHA CC.250 katika maeneo ya mkombezi kata ya mfaranyaki manispaa ya songea walimjeruhi SALGO S/O NDUNGURU kwa risasi mkono wa kushoto na paja la mguu wa kushoto baada ya kumkamatwa kwa kosa la usalama barabarani.

Ameendelezea kueleza kuwa baada ya Agreyi ambaye ni dreva wa pikipiki yenye namba za usajiri T.757 kukamatwa kwa kosa hili ndipo alipompigia simu  kijana huyo ambaye ni majeruhi na kumjulisha kukamatwa kwake na askari kwani yeye ndiye mdhamini wa pikipiki hiyo.

Amesema baada ya kufika kwake eneo hilo ndipo mkusanyiko wa waendesha pikipiki wanaoujilikana kwa jina maarufu kama  bodaboda (YEBO YEBO)ukwa mkubwa na na kuanza kurushiana na askari hao mawe huku majeruhi huyo akiwa ameshika mtutu wa bunduki iliyokuwa imebebwa na askari no G 9800 PC AYUBU na ndipo askari namba G5075PC WAZIRI katika kuinusurusilaha hiyo isiporwe alimpiga sehemu mbili ambazo ni kiganja cha mkono wa kushoto na paja la mguu wa kushoto.

"Upelelezi wa tukio hilo tayari umekwishaanza ili kubaini chanzo  halisi cha tukio hilo na askari husika tunawashikilia kwa mahojiano zaidi ili tuweze kuchukua hatua sitahiki.)alisema kamanada

Aidha amesema mpka hivi sasa majeruhi huyo amelazwa katika hosipitali ya rufaa ya mkoa wa ruvuma ili kupatiwa huduma ya matibu huku hali yake ikiwa inaendelea vizuri.

0 comments:

Post a Comment