Bodi
ya Wakurugeni ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam
(DAWASA) leo Agosti 20,2014 imefanya ziara ya kutembelea Miradi yao ya
Maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini ili kujionea maendeleo ya ukarabati wa
Miradi hiyo miwili ambayo ilikuwa katika ukarabati.Katika ziara hiyo
Bodi hiyo ya DAWASA imeridhishwa na upanuzi wa Mtambo wa Maji wa Ruvu
chini ambao kwa sasa umekamilika kabisa huku ukiwa na uhakika wa kutoa
maji ujazo wa Lita Milioni 270 kwa siku.
Pichani
ni Bango la Mkandarasi anaejenga Visima na kukarabati Mabomba ya Maji
ikiwa ni Kituo kitakachosambaza maji katika maeneo mbali mbali ya Jiji
la Dar es Salaam kutoka kwenye Mitambo ya Ruvu Juu,eneo hili lipo
Kibamba,Jijini Dar es salaam.
Meneja
Miradi wa Kampuni ya Megha Engineering & Infrastructures Ltd ya
nchini India,Murali Mohan (mwenye kizibao cha kijani) ambao ni
wakandarasi wa Ujenzi wa Visima na Ukarabati wa Mabomba ya Maji ya
DAWASA katika eneo la Kibamba,akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Bodi ya
Bodi ya Wakurugeni ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam
(DAWASA) ambayo iko chini ya Mwenyekiti wake,Dkt. Eve-Hawa Sinare (wa
tatu kushoto) wakati walipopita kwenye Mradi huo utakaosambaza maji
kutoka kwenye Mitambo ya Ruvu Juu.
Meneja
Miradi wa Kampuni ya WABAG India,Pintu Dutta (wa pili kushoto) akieleza
jambo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugeni ya Mamlaka ya Maji Safi na
Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA),Dkt. Eve-Hawa Sinare (wa tatu kushoto)
alieambatana na wajumbe wa Bodi hiyo wakati wa ziara yao ya kutembelea
Mradi wa Maji wa Ruvu Juu unaonendelea na ukarabati hivi sasa.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugeni ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es
Salaam (DAWASA),Dkt. Eve-Hawa Sinare (alienyoosha mkono) akielekeza kitu
wakati akiangalia ujenzi wa nyumba za Wafanyakazi wa DAWASA watakaokuwa
wanaendesha miradi hiyo ya Maji Ruvu Juu.
Meneja
Miradi wa DAWASA,Ing. Romanus Mwang'ngo (kulia) akiwaonyesha kitu
Wajumbe wa Bodi ya DAWASA waliofanya ziara ya kutembelea Mirani ya Ruvu
Juu na Ruvu Chini leo Agosti 20,2014.
Ziara ikiendelea.
Mtendaji
Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA),Ing.
Archerd Mutalemwa akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya namna
Shirika lake lilivyojipanga kuwaondolea kabisha hadha ya maji Wakazi wa
Jijini la Dar es Salaam wakati akielezea kukamilika kwa Mtambo wa Maji
wa Ruvu chini wenye Uwezo wa kutoa maji Lita Milioni 270 kwa siku
ukitofautisha na uwezo wa Mtambo wa zamani uliokuwa ukitoa lita chache.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugeni ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es
Salaam (DAWASA),Dkt. Eve-Hawa Sinare akizungumza na waandishi wa habari
juu ya ziara yake hiyo aliyoambatana na Wajumbe wake wote.
Mhandishi
Mshauri wa Kampuni ya UWP,Chacha Wambura (mwenye kizibao cha rangi ya
chungwa) akitoa maelezo ya Maendeleo ya Mradi wa Ruvu chini kwa Ujumbe
wa Bodi ya Wakurugeni ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam
(DAWASA) uliotembelea Mradi huo leo Agosti 2014.
Sehemu ya Mabomba ya kusafirishia Maji katika Mtambo wa Ruvu chini.
Mhandishi Mshauri wa Kampuni ya UWP,Chacha Wambura akifafanua jambo kwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugeni ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka
Dar es Salaam (DAWASA),Dkt. Eve-Hawa Sinare wakati wakitembelea sehemu
ya Mtambo wa Maji wa Ruvu chini uliomalizika matengenezo yake.
Sehemu ya visima vya Maji Ruvu chini.
Makamu
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugeni ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka
Dar es Salaam (DAWASA),Alhaji Said El-Maamry (kushoto) akiuliza jambo
kwa Meneja Miradi wa DAWASA,Ing. Romanus Mwang'ngo (kulia) juu ya Mtambo
wa Ruvu chini,wakati wa ziara yao iliyofanyika leo Agosti 20,2014.Wa
pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo,Dkt. Eve-Hawa Sinare
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugeni ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es
Salaam (DAWASA),Dkt. Eve-Hawa Sinare (wa pili kushoto) akijadiliana
jambo na Makamu wake,Alhaji Said El-Maamry (kulia) mara baada ya
kumaliza ziara ya kutembelea miradi ya Ruvu Juu na Ruvu chini leo Agosti
20,2014.Wengine pichani ni Wajumbe wa Bodi hiyo,Bw. Daniel Machemba
(kushoto) na Ing. Mary Mbowe (wa pili kulia)
Wajumbe
wa Bodi ya Wakurugeni ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es
Salaam (DAWASA) wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza
ziara yao katika Miradi ya Ruvu Juu na Ruvu chini leo.
0 comments:
Post a Comment