Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
Dk.Seif Rashid, akizungumza na wajumbe wa bodi hiyo iliyomaliza muda
wake na mpya wakati akizindua bodi hiyo Dar es Salaam leo asubuhi.
Mganga Mkuu wa Serikali, ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dk.Donan Mmbando akizungumza katika hafla hiyo
kabla hajamkaribisha Waziri kuzindua bodi hiyo.
Mwakilishi wa bodi iliyomaliza muda wake, Profesa .Bakari Lembaritiakitoa neno la shukurani
Mwakilishi wa bodi mpya, Mkurugenzi wa Tiba na Masuala ya Kiufundi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dk.Frank Lekey akitoa neno la shukurani. Kushoto ni Naibu Msajili Hospitali Binafsi Dk.Mahewa Lusinde na Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Dk.Mpoki Ulisubisya.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid (kulia),akimkabidhi cheti cha utumishi wa bodi hiyo,Profesa Bakari Lembariti. Katikati ni Mganga
Mkuu wa Serikali, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dk.Donan
Mmbando. Vyeti hiyo walitunukiwa wajumbe wote waliomaliza muda wao.
Wajumbe wa Bodi mpya wakiwa kwenye
hafla hiyo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Tiba na Masuala ya Kiufundi
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dk.Frank Lekey, Mkurugenzi wa
Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Dk.Mpoki Ulisubisya, Mwanasheria Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Onorius Njole, Mkurugenzi Association of
Private Health Facilities-APHTA na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi-Hospitali
za Umma na Binafsi Idara ya Tiba, Dk.Sijenunu Aaron.
Wajumbe wa bodi iliyomaliza muda wake.
Kutoka kulia ni Profesa .Bakari Lembariti, Profesa Charles Majinge,
Dk.Edda Vahahula, Dk.Jane Kahabi na Dk.Eliuter Samky.
Mkutano ukiendelea.
Mkurugenzi wa Tiba wa Wizara hiyo,
Dk.Margareth Mhando na Mkurugenzi wa Idara ya Uhakiki na Ubora,
Dk.Mohamed wakiwa kwenye mkutano huo.
Katibu wa Bodi hiyo, Dk.Pamella Sawa
akizungumza katika mkutano huo.(Imeandaliwa na mtandao wa habari za
jamii.com-simu namba 0712-727062)
Kaimu Mkurugenzi
Msaidizi-Hospitali za Umma na Binafsi Idara ya Tiba, Dk.Sijenunu Aaron
akiteta jambo na Mkurugenzi Msaidizi wa Vituo vya Umama na Binafsi na
Mwakilishi wa Bodi ya Ushauri ya Hospitali Binafsi Mkoa wa Dar es
Salaam, Dk Ruth Suza.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi iliyomaliza muda wake.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi mpya.
SERIKALI imesema itaainisha ukomo wa
tozo kwa kila huduma inayotolewa kwa kila ngazi ya kituo cha huduma ili
kudhibiti gharama za huduma za afya nchini.
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Afya
na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid Dar es Salaam leo asubuhi wakati
akizindua bodi mpya ya ushauri ya Hospitali binafsi nchini.
Dk. Rashid alisema hatua hiyo imekuja
baada ya kuwepo kwa malalamiko kuhusu huduma zinazotolewa na hospitali
hizo hivyo hatua hiyo itasaidia kuboresha mfumo na kuwatendea haki
wananchi wanaotumia vituo vya kutolea huduma za afya.
"Malalamiko haya ni pamoja na huduma
zisizo na ubora unaotakiwa na gharama zinazotolewa kwa huduma hizo
.Sheria iliyopo inatutaka kudhibiti bei ya huduma hizi kwa kuzingatia
malalamiko haya pamoja na matakwa ya sheria yenyewe," alisema Dk.
Rashid.
Hata hivyo alibainisha kuwa licha ya
kuwepo wa changamoto hizo huduma zinazotolewa na hospitali za watu
binafsi zimechangia katika mafanikio yaliyopatikana katika kufikia
malengo ya maendeleo ya milenia.
Kuhusu bodi hiyo Dk .Rashid aliwataka
wajumbe wapya wa bodi hiyo kufanya vikao vya mara kwa mara vinavyolenga
uboreshwaji wa utoaji wa huduma.Na kuwataka kuendeleza utaratibu wa
kusajili vituo vipya na kufupisha usajili kwa kutmia muda mfupi kwa
kutumia mfumo wa kielektroniki.
Alibainisha kuwa wajumbe wa bodi ya
awali iliyosimamiwa na Mwenyekiti Dk. Deo Mtasiwa imesaidia kuboresha
uwajibikaji wa wahusika hivyo kuboresha huduma na imeokoa maisha ya
wananchi wengi ambayo yangekuwa hatarini endapo bodi isingetekeleza
majukumu yake ipasavyo.
Alitaja wajumbe wa bodi mpya kuwa ni
Dk.Donan Mbando ambaye ni Mwenyekiti, Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa
mbeya Dk. Mpoki Ulisubisya, Mkurugenzi wa Hospitali ya Bugando Profesa
Chalres Majinge, Mkurugenzi wa Tiba na Masuala ya Kiufundi (NHIF), DK.
Frank Lekey.
Wajumbe wengine ni Mkurugenzi Msaidizi-
Hospitali za Umma na Binafsi Idara ya Tiba Dk. Sijenunu Aaron,
Mkurugenzi wa Association of Private Health Facilities (APHTA),
Mwakilishi wa Mkurugenzi, Christian Social Services Comission (CSSC),
Dk.Jane Kahabi na Mwanasheria Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Onorious Njole.
0 comments:
Post a Comment