Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Stephen Wasira (katikati)
alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jana mjini Dodoma juu ya
mkutano wa 30 utakaofanyika nchini mwishoni wiki hii. Kushoto ni Rais wa
Benki ya Maendeleo ya Kusini na Mashariki ya Afrika (PTA), Admassu
Tadesse na kulia ni Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba.
Rais
wa Benki ya Maendeleo ya Kusini na Mashariki ya Afrika (PTA), Admassu
Tadesse (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana
kuhusu mkutano wa miaka 30 ya wanahisa na magavana utakao shirikisha
nchi 18 za Afrika, mkutano huo utafanyika kesho jijini Dar es Salaam.
Katikati ni Waziri wa Ofisi ya Rais (Uratibu na Mahusiano), Steven
Wasira akifuatiwa na Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Stephen Wasira (kushoto)
abibadilishana mawazo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Kusini na
Mashariki ya Afrika (PTA), Admassu Tadesse mara baada ya mkutano na
waandishi wa habari jana mjini Dodoma. Katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya
Fedha Dkt. Servacius Likwelile.
Bodi
ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa
Afrika (PTA) itakuwa mkutano wa mwaka utakaofanyikia nchini jijini Dar
es salaam tarehe 22 mwezi huu.
Hayo
yamebainishwa jana mjini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
(Mahusiano na Uratibu) Stephen Wasira alipokuwa akiongea na waandishi wa
habari juu ya mkutano huo utakaofanyika mwishoni wiki hii.
“Huu
ni mkutano wa kawaida wa mwaka wa Bodi ya Magavana wa nchi wanachama
pamoja na Mawaziri wa Fedha, Tanzania ni mwanachama ndio maana mkutano
wa 30 unafanyika hapa” alisema Wasira.
Wasira
amesema kuwa katika mkutano huo mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwemo
masuala ya fedha na uchumi, maendeleo ya benki ya PTA na mafanikio yake
kwa nchi washirika.
Vile
vile Wasira amesema kuwa PTA ni benki ya Kiafrika na inafanyakazi nzuri
ambapo inaonesha inakua kwa zaidi ya asilimia 30 kwa mwaka kwa miaka
kadhaa hadi sasa na imekuwa na mizania ya Dola za Kimarekani mil. 2.8
ikiwa miongoni mwa benki za maendeleo zinazofanya vizuri katika bara la
Afrika.
Aidha,
Wasira ameongeza kuwa mkutano huo utatanguliwa na semina ya
wafanyabiashara itakayofanyika Agosti 21 siku moja kabla ya mkutano mkuu
wa Magavana hao ambapo Serikali itawakilishwa na Naibu Waziri wa Fedha
Mwigulu Nchemba.
Kwa
upande wake Rais na Mtendaji Mkuu wa benki ya PTA Admassu Tadesse
amesema kuwa Tanzania imekuwa mstari wa mbele na ni mwanachama hai
ambapo imekuwa mfano mzuri kwa nchi wanachama kwa kutoa michango
mbalimbali kwa wakati.
Zaidi
ya hayo, Tadesse amesema kuwa benki hiyo mwaka huu inaadhimisha miaka 30
tangu kuanzishwa kwake, Tanzania imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa
mkutano wa mwaka huu ili washerehekee na Watanzania.
Tadesse
amesisitiza kuwa Benki ya PTA inatoa huduma zake kwa nchi wanachama
ikiwa na lengo la kuwa tasisi ya kifedha inayoongoza Mashariki na Kusini
mwa Afrika katika utoaji wa huduma za kibenki.
Benki
ya PTA ilianzishwa mwaka 1985 ambapo hadi sasa ina jumla ya wanachama 22
ikiwemo nchi 18 ambazo ni Burundi, Comoros, Djibouti Congo, Kenya na
Malawi.
Nchi
nyinine ni Misri, Eritrea, Ethiopia, Mauritania, Rwanda, Seychelles,
Somalia, Sudan, Uganda, Zambia, Zimbabwe na mwenyeji Tanzania
Aidha, PTA inashirikiana na nchi nyingine nje ya bara la Afrika ambazo ni Belarus na China.
Washirika
wengine ni Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), Kampuni ya Bima ya
Mauritia iitwayo Eagle na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Mauritius.
Mkutano
wa mwaka huu unafanyikia Tanzania ikiwa ni utaratibu wa benkiya PTA
kufanya mikutano ya mwaka kwa mzunguko ambapo washiriki watakuwa
Mawaziri wa Fedha, Magavana wa nchi wanachama, sekta binafsi, Mabalozi
wanaowakilisha nchi mbalimbali nchini na Wawakilishi wa Mashirika ya
kimataifa.
0 comments:
Post a Comment