Wednesday, 27 August 2014


 Jembe!jembe!Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla mwenye suti akiwa amebebwa juu na wananchi wa Kijiji cha  Kibati na Pemba wakati wa ziara ya Rais Jakaya Kikwete, mkoani Morogoro jana.


 Amos makalla akihutubia mkutano wa hadhara kibati wakati ziara ya mhe Rais kikwete
KIKWETE amwaga misaada mvomero ni magari ya wagonjwa matatu,fedha za soko na vitanda vya wagonjwa

.MAGUFULI aidhinisha majengo ya mradi barabara wapewe mvomero, daraja kubwa kujengwa na kuongeza fedha

Mbunge wa mvomero na naibu wa maji amewavunja mbavu Rais Kikwete,waziri wa Ujenzi John magufuli na wananchi kwa style yake ya kujenga hoja za mvuto anapoomba kusaidiwa na kila anapoomba alisema baada ya shukrani na mambo mengi mazuri serikali iliyofanya sasa nipige mzinga kwa ajili ya changamoto mbali mbali tulizonazo katika jimbo la mvomero.


Ni katika mkutano wa hadhara kijiji cha kipera mbunge wa mvomero akampongeza Rais kikwete kwa kuwezesha upatikanaji maji na ujenzi wa hosteli na maabara na kumuomba Rais msaada wa magari ya wagonjwa kwa ajili ya kituo cha afya cha melela,mvomero na Mlali alisema"mhe Rais nikushukuru kwa mambo mazuri uliyoyafanya katika jimbo langu husani utatuzi wa kero kubwa ya maji, umeme na ujenzi wa hii hosteli na maabara ila mzee naomba nikupige mzinga kidogo muendelezo wa mzinga wa vitanda unehaidia,mzinga nilikupiga wa barababara ya lami mzumbe mpaka Nyandira amekubali sasa nisaidie magari  matatu ya wagonjwa kwa ajili ya vituo vya afya vya melela , mvomero na mlali"


Katika kijibu Rais kikwete alisema mnaye mbunge mzuri hodari wa kupiga mizinga kwa mambo ya maendeleo maombi yake yote nimeyapokea na nitayafanyia kazi.


Katika siku ya pili ya ziara katika kijiji cha mvomero wakati wa uwekaji jiwe la msingi wa barabara ya magole Turiani Mziha na mkutano wa kijiji cha Kibati alipopewa nafasi alipongeza sana  kazi nzuri zilizofanywa na serikali ikiwemo ujenzi wa barabara ya Magole mziha,matengenezo makubwa ya barabara ya Lusanga  Kibati , ujenzi wa minara, miradi ya maji vijiji vya Kwadoli,Pemba,msolokelo na kibati pamoja na kituo cha afya kibati  na katika kuhitimisha alimalizia kwa kusema"mhe Rais na mhe waziri wa ujenzi serikali imefanya mambo makubwa nawashukuru nimalize kwa mizinga na leo naomba serikali mara mradi wa kujenga hii barabara yetu ya magole mziha naomba majengo ya wasimaizi mradi tukabidhiwe tuyatumie kwa ajili ya Veta au kituo cha Afya na pamoja na kazi nzuri ya matengenezo mazuri ya barabara ya Lusanga kibati  na kuongeza kuhudumia barababara ya kibati hadi Tunguli (kilindi) sasa kwa heshima niombe Tanroad watujengee daraja kuunganisha kijiji cha pandambili na kilindi na kuhudumia barabara ya kuanzia Kibati  hadi Diburuma"


Katika kujibu maombi hayo Waziri Magufuli  alikubali kukabidhi majengo,kujenga daraja na kuongeza kuhudumia barabara zilizoombwa na Rais Kikwete alikubali na kusema makala ananipiga sana mizinga lakini jambo jema anaaomba mambo ya maendeleo tutamsadia

0 comments:

Post a Comment