Friday 8 August 2014

WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, ameusifu Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa daraja la Kigamboni.


Ujenzi wa daraja hilo umekamilika kwa asilimia 60 ambapo mpaka sasa NSSF imetoa sh. bilioni 117 kati ya Bilioni 214 zitakazokamilisha ujenzi wa daraja hilo.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam, alipotembelea daraja kuona namna ujenzi unavyoendelea, Dk. Magufuli alisema kuwa ujenzi wa daraja hilo umekutana na changamoto nyingi ikiwemo kina kilichokuwa katikati ya bahari kupoteza malighafi ya ujenzi ambapo wahandisi waliamu kufanya utafiti.

Alisema kuwa juhudi za NSSF  katika kufadhili mradi huo umewezesha changamoto zilizokuwa zikiukabili maradi huo kufanyiwa kazi.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa NSSF, Ludovick Mrosso, alisema kuwa mradi huo unatarajiwa kukamilika Julai, 2015 ambapo katika daraja zitakuwa barabara sita za magari, mbili za wapita kwa miguu.
Maradi huo unajengwa kwa kushirikisha Wizara ya Ujenzi, NSSF na Tanroads. 
Msafara wa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli ukiwa katika ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni linalojengwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa kushirikiana na Serikali.  
 Waziri wa Ujenzi, John Magufuli (katikati), akikagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni.
Waziri wa Ujenzi, John Magufuli akisalimiana na mafundi katika eneo la ujenzi.
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (wa pili kulia) akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni kutoka kwa Meneja wa Mradi wa ujenzi wa daraja hilo, Mhandisi Kareem Mataka, wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja hilo.
 Mh. Magufuli akifafanua akitoa maelekezo kwa Mhandisi Kareem Mataka (kulia).
 Wavuvi wakivua samaki katika eneo la mradi wa ujenzi wa daraja hilo.
 Mhandisi wa Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Kareem Mataka akitoa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo kwa Waziri wa Ujenzi John Magufuli alipofanya ziara kujionea maendeleo ya daraja hilo.
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (wa pili kulia) akikagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni linalojengwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii  (NSSF), kwa kushirikiana na Serikali. Kulia ni  Meneja Mradi ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Kareem Mataka.
 Waziri akiwa katika zira ya ukaguzi pamoja na maofisa kutoka Wizara ya Ujenzi, NSSF pamoja na waandishi wa habari.
 Ukaguzi wa Daraja.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ludovick Mrosso akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni.
 Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni. Kushoto ni Mkurugenzi wa Miradi wa NSSF, Yakub Kidula. 
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (kulia), akimpongeza Meneja Mradi ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Kareem Mataka mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo.
 Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli akimshukuru Kaimu Mkurugenzi wa NSSF,  Ludovick Mrosso kutokana na kazi nzuri inayofanywa na NSSF katika ujenzi wa daraja la Kigamboni.
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli akibadilishana mawazo na Meneja wa Mradi wa Daraja la Kigamboni, Kareem Mataka, Mkurugenzi wa Miradi wa NSSF, Yakub Kidula (katikati), baada ya kufurahishwa na maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni.

0 comments:

Post a Comment