Watu saba wamekamatwa Jijini Arusha kwa tuhuma za kuhusika kwenye mauaji ya unyang’anyi wa kutumia silaha kwa wanawake.
Wanadaiwa pia kusababisha kifo cha mtoto, Christen Nickos mwenye umri wa miaka mitatu na nusu mkazi wa Olasiti hapa.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Arusha, Liberatus Sabas alisema watu wawili kati ya saba ambao ni
Japhet Lomnyaki (25) mkazi wa Sakina na Nehemia Kweka (34) mkazi wa
Ngaramtoni walifikishwa mahakamani juzi.
Alitaja
wengine, Adam Mussa (30) mkazi wa Majengo, Tito Loomoni (25) mkazi wa
Shamsi, Joseph Loomoni (29) mkazi wa Shamsi, Abdallah Maglan (22) mkazi
wa Oldadai na Emmanuel Maglan (23) wa Oldadai wanaendelea kuhojiwa na
polisi.
Alisema
wanatuhumiwa kuhusika kwenye tukio la Agosti 21 mwaka huu maeneo ya
Olasiti ambako wakiwa na pikipiki aina ya Toyo , walimjeruhi kwa kumpiga
risasi mtoto Christen sehemu ya mdomo na kusababisha kifo chake.
Wanatuhumiwa
pia kuhusika kwenye tukio lingine la mauaji ya mwanamke Shamimu Yulu
(30) maeneo ya Sakina kwa Idd ambaye alipigwa risasi na kufariki dunia
akiwa anapatiwa matibabu hospitali ya Selian.
Mwanamke
mwingine Flora Porokwa alilazwa Hospitali ya Arusha Lutheran Medical
Centre (Selian) baada ya kupigwa risasi ya bega kwenye tukio lingine
tofauti likihusisha watu waliokuwa kwenye pikipiki.
0 comments:
Post a Comment