Sunday 24 August 2014

Wananchi wa  kijiji  cha Luvuyo kata ya Madope  wakimpokea  mbunge wao Deo Filikunjombe kwa maandamano
Wanachama  wa  chama  cha mapinduzi (CCM)   pamoja na  wananchi wa  kijiji cha Luvuyo kata ya Madope  wakishirikiana jana na mbunge  wao Deo Filikunjombe  (kushoto) kuchimba mifereji ya  maji katika barabara ya Luvuyo - Njombe  yenye urefu wa Kilomita 6 ambayo inajengwa kwa  ufadhili wa mbunge huyo kwa kiasi cha zaidi ya Tsh milioni 50
Wananchi wa  Luvuyo wakimsikiliza  mbunge  wao Deo Filikunjombea
Mbunge wa  jimbo la Ludewa akiwahutubia  wananchi wa Luvuyo mara  baada ya  kuzindua  ujenzi wa barabara ya Luvuyo - Njombe
Mbunge  wa  jimbo la  Ludewa  Deo Filikunjombe akisafirishwa katika  katika mkokoteni waw  kukokotwa na  ng'ombe  baada ya  wananchi  wa  kijiji  cha Luvuyo kata ya Madope  ambao awali  walitishia  kuhama  wilaya ya  Ludewa  kuhamia Njombe kusikilizwa  kilio  chao  cha ubovu wa  miundo mbinu kwa  kuanza kujengewa barabara na  mbunge   huyo
WANANCHI wa kijiji cha Luvuyo kata ya Madilu wilaya ya Ludewa mkoani Njombe ambao awali walitaka kuhamia wilaya ya Njombe kutokana na Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kuwatelekezea barabara ya Luvuyo – Njombe wamempongeza mbunge wao Deo Filikunjombe kwa kuwajengea barabara hiyo na kubadili uamuzi wao wa kuhamia Njombe. 

 Wakizungumzakatika hafla ya mbunge Filikunjombe kuzindua ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa zaidi ya 6 inayojengwa kwa zaidi ya milioni 52 ,walisema kuwa awali walipata kuandika barua katika uongozi wa Halmashauri hadi kwa waziri mkuu wakiomba kuhamia wilaya ya Njombe kutoka na kijji hicho kuwa kama kisiwa kutokana na ubovu wa barabara . 

Mmoja kati ya wananchi hao Apudencia Lugome alisema kuwa wananchi hao walifikia hatua ya kuandika barua ya kutaka kijiji hicho kuwa sehemu ya wilaya ya Njombe kutokana na viongozi wa wilaya ya Ludewa kushindwa kuwatekelezea maombi yao ya ukarabati wa barabara ya kijiji hicho toka nchi ipate uhuru Kwani alisema kuwa mbali ya kujengwa kwa barabara ya Njombe – Ludewa ila wao katika kijiji hicho barabara hiyo ilikuwa si msaada kwao zaidi ya ile ya Luvuyo – Njombe ambayo hutumia kusafirisha mazao yao na ni tegemeo katika usafiri hivyo kitendo cha Halmashauri ya Ludewa kupuuza kilio chao ni kuwafanya wananchi hao kujisikia kama wapo katika kisiwa . 

 Hivyo alisema hatua kutoka na hali hiyo wao wenyewe wananchi walilazimika kuchangishana fedha kiasi cha Tsh 50,00 kila mmoja na kupata kiasi cha Tsh milioni 3.6 kwa ajili ya kuanza kutengeneza maeneo korofi kabla ya mbunge wao kufika katika mkutano wake na kuamua kuchukua jukumu ya kujitolea kujenga barabara hiyo yote . 

 “Tunashukuru sana mheshimiwa mbunge wetu na jembe kwa wana Ludewa kwani toka nchi yetu ipate uhuru Ludewa hatujapata kuwa na mbunge makini kama wewe hivyo hatuna sababu ya kuhangaika na mtu mwingine mwaka 2015….kwani mwenye kutatua kero zetu zaidi yako hakuna “ 

Huku diwani wa kata hiyo Godfrid Mhagama wa kata ya Madope akieleza kuwa sababu ya wananchi hao kufanya maandamano na kumpokea kwa usafiri wa ng’ombe ni kutokana na heshima kubwa ambayo mbunge huyo ameionyesha kwao wana kata ya Madope hasa wananchi wa kijiji cha Luvuyo . 

 Alisema kuwa barabara hiyo imekuwa kero kiasi cha wananchi hao kuwakimbiza watendaji wa Halmashauri ambao walifika katika kijiji hicho kwa ajili ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo.

 “Kweli suala hili kwetu limetuumiza sana kichwa ilifika sehemu wakuu wa idara walikuwa hawafiki katika kijiji hiki kutokana na wananchi kuwa na jazba iliyotokana na ubovu wa miundo mbinu na ahadi zisizotekelezeka za Halmashauri yetu” 

Katibu wa itikadi na uenezi CCM mkoa wa Njombe Onolatus Mgaya mbali ya kumpongeza mbunge huyo na wananchi kwa kuunganisha nguvu zao bado aliwataka wananchi hao kutunza barabara hiyo ambayo kukamilika kwake ni ukombozi mkubwa kwao . 

Alisema kuwa wapo baadhi ya viongozi wamekuwa wakiangalia misaada inayotolewa na Mbunge huyo kwa macho matatu ambapo baadhi hujikuta wakiiba na kufanya ni mali yao binafsi kitu ambacho si kizuri bali wananchi washirikiane na viongozi hao kuhakikisha wanailinda na kuisimamia misaada wanayopewa iliiweze kuwanufaisha wote 

 “…Nampongeza sana Mbunge kwa misaada mbali mbali aliyotoa kwa wananchi wake kwani amejitahidi kuweza kutatua kero mbali mbali zinazowasumbua wananchi katika sekta ya afya, elimu ,m iundombinu na kilimo, naomba tuitunze na itumiwe na wananchi wote,"alisema Mgaya

 Huku Filikunjombea mbali ya kuzindua ujenzi wa barabara hiyo pia alikabidhi msaada wa bati 200 ya geji 28 mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wwa nyumba ya mganga wa Zahanati ya Luvuyo na ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi katika shule za msingi kijijini hapo pia toroli na spendi kwa ajili ya kikundi cha vijana wanaojishughulisha na uoteshaji miti kijijini hapo bado aliwataka kuendeleza umoja zaidi . 

Kwani alisema iwapo wananchi hao wataendelea kujitolea zaidi yeye kama mbunge wao atazidi kuwwaunga mkono na kuwahakikishia kuwa kamwe hatawaangusha katika utendaji kazi wake na kuwa siku zote anaamini kuwa mwwajiri wake ni mpiga kura na si vinginevyo. 

 " Ndugu zangu wana Luvuyo nawapenda sana baada ya kuja wiki iliyopita hapa na kufanya mkutano kweli nilivutiwa sana na jitihada zenu ndio maana nilikubali kuwasaidia kujenga badaraba hii kwa zaidi ya Tsh milioni 52 ila nawahakikishia fedha hizi hazijatoka mfukoni mwangu ila kutokana na kuishi na watu vema nimewaomba mitambo nja mafuta ya kuja kusaidia ujenzi huu baada ya kuvutika na jitihada zenu"

0 comments:

Post a Comment