Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Hussein Ngaga. |
OFISA
ushirika wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma,
Raphael Luvanda ameonja joto ya jiwe baada ya Wanachama wa chama cha kuweka na
kukopa, Mbinga Lutheran SACCOS kumjia juu na kumweleza kwamba hawana imani naye
katika utendaji wa kazi zake hivyo hawamtaki kumuona akifanya kazi za ukaguzi
katika umoja huo.
Sambamba
na hilo
wanachama hao ambao walionekana kukerwa na tabia za Ofisa ushirika huyo
walisema, sababu zao za msingi za kumkataa wamekuwa wakimtuhumu kwa muda mrefu
kwamba anafanya kazi zake kwa mrengo wa kushoto na sio kwa maslahi ya
wanachama.
Walieleza
kuwa bodi husika itazifikisha tuhuma husika kwa mwajiri wake ambaye ni
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo, ili ziweze kufanyiwa kazi huku
wakitaka kuanzia sasa shughuli za ukaguzi zifanywe na ofisa ushirika mwingine
na sio vinginevyo.
Hali
hiyo ilijitokeza katika mkutano mkuu wa wanachama hao uliofanyika juzi mjini
hapa, kwenye ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Walisema
katika hali ya kusikitisha Luvanda amekuwa na tabia za ajabu hataki kufuata
taratibu zake za kazi, badala yake amekuwa mtu wa kupenda kuzua migogoro ya
hapa na pale kati ya uongozi wa SACCOS hiyo na wanachama kwa ujumla.
Vilevile
katika taarifa yake ya ukaguzi ya mwaka 2013 alishindwa kubainisha wizi wa
fedha uliofanywa na aliyekuwa mhasibu wa ushirika huo, Ansilla Kapinga na
kusababisha uongozi husika kutumia gharama kubwa kuleta wakaguzi wengine kutoka
nje ya wilaya ya Mbinga.
Waliongeza
kuwa alifikia hatua, vitabu na nyaraka muhimu za umoja huo alizizuia ofisini
kwake akitaa kuzirejesha jambo ambalo lilikuwa likizua malalamiko ya hapa na
pale miongoni mwa wanachama na kufanya wakose imani naye.
“Kwa
mwenendo huu hatutaweza kuvumilia suala hili, ni vyema ofisa ushirika huyu
afanye kazi zake kwa kufuata taratibu zilizowekwa na sio kujenga mipasuko
ambayo inavuruga ushirika wetu”, walisema.
Walifafanua
kuwa wanazo taarifa kwamba, Luvanda amekuwa hata akitoa taarifa za upotoshaji
kwenye maeneo mengine ya mashirika ambayo yanatoa mikopo hapa wilayani, kwa
lengo la kugonganisha viongozi husika na wanachama kwa maslahi yake binafsi.
Hata
hivyo kwa upande wake Ofisa ushirika huyo alipopewa nafasi ya kujieleza
aliishia kwa kuwaomba radhi wanachama hao, na kuondoka bila kutolea maelezo
yakinifu yenye kufikia muafaka wa tuhuma ambazo alinyoshewa kidole.
0 comments:
Post a Comment