Friday 5 September 2014

ZAIDI ya wakazi 100 wa Kijiji cha Hondogo, Kata ya Kibamba wilayani Kinondoni Dar es Salaam wanalala nje baada ya nyumba zao kubomolewa na mabaunsa.
 
Akizungumza na …… jijini jana, mmoja wa wakazi wa eneo hilo Vitalis Muro, alisema  tukio hilo limetokea Septemba mosi mwaka huu na kwamba nyumba zilizobomolewa ni 16.
 
Alisema, mabaunsa hao walibomoa nyumba hizo baada ya kuagizwa na mtu aliyetajwa kwa jina la Prosper Liaruu ambaye anadai kuwa eneo hilo la kwake.
 
Muro, alisema kauli ambayo ilipingwa na wakazi hao, wakidai kuwa walijenga nyumba hizo tangu mwaka 2003 baada ya kupewa viwanja hivyo na serikali ya kijiji hicho tena kwa barua.
 
“Tunachoshangaa tangu tumepewa maeneo haya mwaka 2003 hatujamuona mtu huyo na wala hatumjui, kama tulikuwa na makosa kama anavyodai basi angetufungulia kesi mahakamani kitendo ambacho hajafanya,”alisema Muro.
 
Diwani wa Kata ya Kibamba Issa Mtemvu, alisema suala hilo sio geni bali ni kesi iliyozaliwa na uamuzi  wa serikali wa mwaka 2003 wa kunyang’anywa mapori baadhi ya watu waliyoshindwa kuyaendeleza kwa kipindi cha miaka mitano ambapo Learu alikuwa miongoni mwao.
 
Alisema baada ya kugawanywa mapori mbalimba ikiwemo hilo la heka sababa ambalo Liaruu anadai kuwa lilikuwa lakweke, hakuridhishwa na uamuzi huo hali iliyomfanya akafumgua kesi katika Baraza la Kata.
 
Mtemvu alisema kesi hiyo ilisikilizwa na uamuzi ulikuwa ni kwamba wananchi hao waendelee kuishi katika maeneo hayo ambapo yeye aliachiwa heka moja na nusu baadala ya tatu katika sabab kama alivyokuwa ameahidiwa na serikali.
 
Hata hivyo, Learuu hakuridhika na uamuzi huo, akamua kwenda mbele kufungua kesi tena mahakamani dhidi ya Abdallah Kaisi na wengine ambako Agosti Mosi mwaka huu alishinda kesi hiyo na ndipo juzi Septemba Mosi akaamua kuchukuwa uamuzi huo.
 
Mbunge wa Ubungo, John Nyika, alikutana na wakazi hao, alisema kuupatia ufumbuzi mgogoro huo ni vema Waziri wa Ardhi anamtaka Waziri wa Ardhi, na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, aende Hondogo-Kibamba na Kwembe-Mloganzila  kukutana na wananchi hao wenye migogoro ya ardhi.
 
Alisema, kuachiwa kwa migogoro hiyo kuendelea bila ya kupatiwa ufumbuzi katika maeneo hayo kumesababisha kuleta madhara ya kibinadamu.
 
Aidha, alivitaka vyombo vya dola kuwa vinahakikisha vinafuatilia kwa karibu chanzo cha mgogoro huo, ili watakaobainika wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

0 comments:

Post a Comment