Friday 22 August 2014

SCHO.3_563bd.jpg
WALIMU wa shule ya sekondari ya Kihesa iliyopo manispaa ya iringa wameendesha mgomo wa siku mbili kutoingia madarasani kufundisha wakimshinikiza Ofisa elimu taaluma manispaa ya iringa kufika shuleni hapo na kumuondoa mwanafunzi aliyefukuzwa shule na bodi kwa makosa ya utomvu wa nidhamu.
Mgomo huo ulichukua takribani masaa sita shuleni hapo ambapo Mwanafunzi huyo aliyetambulika kwa jina Lomina Chengula kidato cha Pili D akiwa na wenzake mapema mwezi huu alisimamishwa masomo na uongozi wa bodi ya shule hiyo kwa makosa yasiyovumilika, lakini kioja kilijitokeza pale ofisa elimu taaluma huyo kuchukua jukumu la kumrejesha shuleni mwanafunzi huyo kwa nguvu.
Awali katika sakata la utovu wa nidhamu walikuwa wanafunzi tisa na bodi iliamua kuwarejesha wanafunzi tisa kwa masharti maalumu na kati ya hao tisa wengine wapo madarasani hadi sasa na stafu ya kihesa haina tatizo na hao wanafunzi kutokana na bodi kuamuru warudi shuleni,ila lililoleta msuguano hapo ambalo linapelekea walimu kutoingia madarasani mpaka watakapopata ufumbuzi wa swala hilo ni juu ya binti mmoja ambae bodi ya shule ambae ndiyo mwakilishi wa kamishina wa elimu iliamuru uyo binti na wenzake kwa sababu walikuwa katika makundi wasimamishwe shule ofisa elimu taaluma kwa mamlaka yake na sisi tunajiuliza ameyapata wapi amembeba mtoto yule hatujui ni kwa urafiki wake na huyo ama ni urafiki gani na familia ya huyo mtoto, lakini alimleta shuleni na kumshinikiza makamu mkuu wa shule amruhusu mtoto arudi shule kusoma lakini tulipopata taarifa tulijiuliza hii itakuwa ni kinyume na haki na vilevile ni kudharau bodi ya shule na ofisa elimu hana mamlaka ya kuwarudisha wanafunzi waliofukuzwa na bodi.
Akizungumzia kitendo hicho mmoja wa walimu shuleni hapo alisema kuwa pamoja na kuendelea na msimamo wa kutoingia madarasani ameutaka uongozi wa juu akiwemo mkuu wa mkoa kuingilia suala hilo kisheria na kuchukua hatua stahiki kwa kulinda maadili ya kazi ya ualimu.
Kwa mujibu wa malalamiko ya walimu hao ni juu ya ukubwa wa makosa yanayomkabili mwanafunzi huyo ambaye kwa taratibu hayawezi kuvumilika katika taasisi yoyote ya elimu nchini kutokana na baadhi ya makosa kuingilia maslahi na usalama wa familia za jamii inayowazunguka.
Baadhi ya makosa ambayo mtoto huyo anaidawa kuyafanya ni pamoja na alifumaniwa mtaani na mume wa mtu kesi yake ikaenda hadi polisi na hapa shuleni ana kesi ya wizi na kesi ya uzinifu uthibitisho upo na alikiri kwa barua hayo ni baadhi ya makosa ambayo binti alitenda na bodi iliomba uthibitisho ofisi ya nidhamu kwa kushirikiana na stafu ya kihesa ilipeleka viambatanisho bodi na bodi iliridhia kwamba mwanafunzi huyo kwa viambatanisho kupelekwa pamoja na baba yake mzazi kukiri kwamba akikamatwa na kosa lingine afukuzwe lakini kinachoshangaza ni kwamba kwa nini mwanafunzi huyo alifanya makosa kama ya kudhalilisha shule.
Pili mamlaka ya ofisa huyo katika kumrudisha mwanafunzi shuleni hana mamlaka hiyo, alitakiwa kuomba bodi labda aangalie kibinadamu, lakini alishindwa kufanya hivyo ameamua kutumia mamlaka yake kumdhalilisha mkuu wa shule ya kihesa bodi ya kihesa sekondari na walimu wote wa shule hiyo na hatujui ni kwa sababu gani alifanya hivyo na tungependa kujua kwamba anajua mamlaka yake na mipaka yake na sisi tumeasmua hatutaingia madarasani hadi atakapokuja kumchukua mwanafunzi huyo, alihoji.
Tunataka aje amchukua huyu mtoto pili atuombe radhi sisi walimu wenzake Kwa sababu anatumia cheo chake vibaya tatu amekurupuka kwa sababu sisi walimu tuna kazi kubwa kama mbili za kumsaidia mtoto kumlea pamoja na kumfundisha haiowezekani mtoto kufanya makosa makubwa ya kumfukuzisha shule tumekaa walimu,bodi ya shule walimu wa nidhamu,kamatiu ya nidhamu na jopo lote la walimu halafu bodi kumtoa halafu yeye anakuja kumrudisha hiyo ni kutudhalilisha sisi walimu hatupo tayari kukubali mwanafunzi aliyefukuzwa na bodi kurudi shuleni.
" Sisi kama walimu hao tumeshikilia msimamo wetu wakidai kudhalilishwa na maamuzi ya kiongozi huyo huku wengine wakijenga hoja juu ya uhalali wa Ofisa huyo kushika madaraka kutokana na rekodi mbaya ya uongozi aliyokuwa nayo tangu awali mwanafunzi huyo ."alisema mmoja wa walimu shuleni hapo.
Kwa upande wa uongozi wa serikali ya wanafunzi dada mkuu wa shule hiyo Neema Mtisi alisema kuwa maamuzi ya bodi yalikuwa sahihi na kwa muda huo kama viongozi walikuwa kwenye pilika za kumwandikia barua mkuu wa mkoa kufikisha kilio cha kukosa masomo kwa siku mbili mfululizo.
Hata hivyo mtandao huu ilimtafuta Ofisa elimu taaluma huyo ili kuthibitisha sakata hilo lakini ziligonga mwambakutokana na kupokea simu lakini hakuongea na baadae kuzima simu mojakwa moja wakati huo nipashe iliendelea kumtafuta mkurugenzi wa manispaa hiyo naye alisema kuwa yupo ziarani mkoa wa arusha akirudi ataliongelea suala hilo.

0 comments:

Post a Comment