MAPIGANO
yakurushiana mishale,mawe na marungu yanayohusishwa na kugombea ardhi,
yameibuka kati ya wananchi wa Kijiji cha Sirorisimba wilaya ya Butiama
na Kijiji cha Mikomariro wilaya ya Bunda mkoani Mara na kusababisha
baadhi ya wananchi kujeruhiwa kwa kuchomwa mishale na kukimbia makazi
yao.
Tukio hilo limekuja
kufuatia madai ya kuwepo kwa mgogoro wa muda mrefu wa ardhi baina ya vijiji vya
wilaya hizo mbili huku ukimya wa viongozi wa wilaya ukitajwa kuwa chanzo cha
kuibuka kwa mapigano hayo.
Wakiongea na Blog hii baadhi ya wananchi wa kijiji cha Sirorisimba wilaya ya Butiama
mkoani Mara wamesema mgogoro huo umeanza miaka mingi iliyopita ambapo wananchi
kutoka kijiji cha Mikomariro wilaya ya Bunda wamekuwa wakivamia wananchi wa
kijiji hicho lakini mpaka sasa hakuna hatua zinazochukuliwa na viongozi wa
wilaya hiyo.
Walisema uvamizi wa
maeneo makubwa uliofanywa hivi karibuni katika eneo hilo umesababisha mapigano
makali na kusababisha mtu mmoja kuchomwa Mshale mgongoni na kulazwa kwenye
hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara.
Mmoja wa majeruhi aliyechomwa mshale kwenye tukio hilo na kulazwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara Hamisi Nyahanga amesema alivamiwa kwenye eneo lake la kilimo na wananchi na kuambiwa siku zake za kuishi zimekwisha na kuamua kukimbia ndipo alipopigwa mshale wa mgongo
0 comments:
Post a Comment