Wednesday, 30 July 2014

Ziwa Nyasa limezungukwa na nchi tatu ambazo ni Tanzania,Malawi na Msumbuji.Ziwa hilo lipo kwenye usawa wa meta 500 toka usawa wa bahari, kina cha ziwa hilo ni karibu meta 750,urefu wake ni karibu  kilometa 1000,upana mkubwa ni kilometa 80 na upana mdogo ni kilometa 15.Huku tafiti mbalimbali zikionesha kuwa ziwa hulo ndilo zuwa pekee linaongoza kwa aina za samaki ,na kutokana na utafuti ambao umefanyika katika ziwa Nyasa upande wa Tanzania na Malawi umebaini kuwa ziwa hilo linaoongoza ulimwenguni kwa kuwa na aina nyingi za samaki ukilinganisha na maziwa mengine duniani.

Kulingana na utafiti ambao ulifanywa na jumuiya ya nchi zilizo kusini mwa Afrika(SADC) kwa kushirikiana na  nchi ya Uingereza kwenye ziwa Nyasa kati ya mwaka 1991 hadi 1994 na mwaka 1996 hadi 2000,ulionesha kuwa ziwa hilo lina kiasi cha tani 165,000 za samaki na kati ya kiasi hicho tani 35,000 za samaki ni jamii ya samaki wa maji ya juu ambao wanaweza kuvuliwa bila kuathiri uvuvi kila mwaka. 

Licha ya tafiti hizo lakini wavuvi wa mwambao huo hawana Kikosi cha Polisi cha Wanamaji wa kuweza kusaidia uokozi wa majanga yanayotokea Ziwani.PITIA BAADHI YA PUCHA HIZI.

Hiyo ni hali halisi kwa Wakazi wa Mwambao wa Ziwa Nyasa wanavyokabiliana na hali ya Majanga yanayotokea Ziwani, hakuna Uokozi wa uhakika bali kutumia zana za Asili katika kuwaokoa watu wanaopatwa na majanga katika Ziwa Nyasa.
Vijana wa uokoaji katika Mwambao wa Ziwa Nyasa wakitoka kuwaokoa Vijana wawili waliozama kwenye Maji, Yohana Behewa na john Behewa waliozama Kilindini kilometa 20 kutoka nchi kavu katika maeneo ya Kijiji cha Chiulu Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma .
Vijana wa Uokozi wakivuta Mtumbwi uliowaokoa vijana waliokuwa wamezama kutokana na kupigwa na Wimbi wakati wa Dhoruba kali wakati wakiwa Ziwani.
Hapo ni vijana waliookolewa wakiwa wamefikishwa Nchi kavu ambako walipatiwa msaada baada ya kuokolewa na vijana wenzao huku wakiwa wamechoka kutokana na kunywa  maji.
Kikosi cha ukoaji Kilichopo Kijiji cha Chiulu wakivuta mtumbwi uliobeba watu waliowakoa kutoka Ziwani baada ya kupigwa na dhoruba na kuzama majini hali iliyotokana na matumizi ya Zana hafifu ambazo hazikidhi kwa kushindana na Mawimbi makali yanayo tokana baada ya  Dhoruba kali  inapotokea katika Mwambao wa Ziwa Nyasa. Wananchi wa Mwambao wa Ziwa Nyasa wamesema hali hiyo imekuwa ikitokea mara kwa mara na hakuna njia nyingine inayotumika kuokoa wahanga wanaopatwa na kadhia hiyo zaidi ya kutumia vifaa duni walivyonavyo.

0 comments:

Post a Comment