Mgeni
rasmi Mkuu wa Wilaya Kilolo Gerald Guninita akilakiwa na viongozi
mbalimbali wa mkoa wa Iringa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa
yaliofanyika kimkoa katika Kijiji cha Lugalo wilayani Kilolo leo. Mkuu
wa wilaya huyo alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine
Ishengoma. Kumbukumbu ya mashujaa huadhimishwa kila mwaka Julai 25,
ambapo mashujaa waliopigana katika vita ya kuikomboa nchi kutoka katika
utawala wa wakoloni. Sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa
zilifanyika kitaifa katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam
na Mgeni Rasmi Rais Jakaya Kikwete.
Mgeni
rasmi Mkuu wa Kilolo Gerald Guninita akiweka ngao ya jadi katika mnara
wa mashujaa wa jeshi la Chifu Mkwawa, mnara huo upo karibu na
walipozikwa askari wa kijerumani 300 wakati wa vita vya Mkwawa mwaka
1891 wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yaliofanyika kimkoa
katika Kijiji cha Lugalo wilayani Kilolo leo.
Mshauri wa mgambo Mkoa wa Iringa, Meja E.M. Akili akiweka upinde kwenye mnara wa mashujaa.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Iringa ACP, Ramadhani Mungi akiweka silaha ya jadi
(mkuki) kwenye mnara wa mfano wa mashujaa. Mnara wa mashujaa wa askari
wa Chifu Mkwawa utarajia kujengwa mahali hapo karibu na mnara wa
wajerumani 300 waliozikwa katika Kijiji cha Lugalo wilayani Kilolo, Mkoa
wa Iringa.
Mwanajeshi mstaafu, Magnus H. Mpinge akiweka silaha ya jadi (shoka) katika mnara.
Mzee wa jadi Constantino Mlawa akiweka sime kwenye mnara.
Askari wa
Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakifwatua risasi za baridi
hewani mara tatu kama ishara ya kuwakumbuka mashujaa wetu. (PICHA ZOTE NA FRIDAY SIMBAYA)
0 comments:
Post a Comment