Wednesday 20 August 2014




KITENGE WAKATI AKIKABIDHIWA MKATABA MPYA WA E FM.


Mtangazaji mpya wa E FM Radio, Maulidi Kitenge anatarajia kuanza kusikika tena hewani kesho Alhamisi.

Kitenge maarufu kama jezi namba 10 mgongoni anatarajia kuanza kusikika katika kipindi kipya cha redio hiyo ambacho kitakuwa kikirushwa saa 1 usiku, kila siku.

Akizungumza , Kitenge ambaye ni mtangazaji maarufu wa michezo nchini alisema wako katika maandalizi ya mwisho kabla ya kuanza kipindi hicho saa moja kamili kesho Alhamisi.
 
“Maandalizi yanakwenda vizuri na Mungu akijaalia, Alhamisi tutaanza,” alisema Kitenge.

Kitenge na mtangazaji pacha wake, Katanga wamehamia E FM wakitokea Radio One.
 
Kitenge akifanya kazi Radio One kwa miaka 14 ,na siku nne zilizopita aliaga rasmi na kuanza makazi mapya na redio hiyo mpya.

0 comments:

Post a Comment