Sunday, 10 August 2014

 



Ukatili dhidi ya wenye ulemavu wa ngozi (Albino) umejitokeza tena mkoani Tabora ambapo mtoto Pendo Sengerema (14) mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Nundu, amekatwa mkoni wake wa kulia na wahalifu kukimbia nao kusikojulikana na aliyeshiriki uharifu huo akihaidiwa kulipwa laki tisa huko katika kijiji cha Usinge wilayani Kaliua.Akiongea kwa tabu alipolazwa katika hospitali ya wilaya ya Urambo majeruhi Pendo Sengerema amesema kuwa, aliyemkata mkono alimfahamu maana ni jirani anayesadikiwa kuwa, ni mganga wa kienyeji, ambapo kaimu mganga wa hospitali hiyo, Doct James Kang’oma, akidai kuwa walijitahidi kuokoa maisha yake kutokanana kutoka kuvuja damu nyingi.

Mratibu wa chama cha wenye ulemavu wa ngozi wilaya za Urambo na Kaliua Bw Focus Mgesera, amesema kuwa, pamoja na mtoto huyo kulazwa katika hospitali hiyo bado kuna hali ya hatali kwake kwani kwa namna moja ama nyingine anaweza kuuawa kutokana na kuwafahamu waliomjeruhi, hivyo anahitaji ulinzi.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Under the same sun, Bi Vicky Ntetemya aliyefika hospitalini hapo kumwona mtoto huyo amesema kuwa, serikali iwe makini na jamii ya wenye ulemavu wa ngozi kutokana na masuala ya wagombea nafasi za uongozi kujishirikisha ma mambo ya waganga wa kienyeji.
Chama cha walemavu wa ngozi nchini kimeraani tukio hilo kikitaka serikali kuongeza ulinzi kwa jamii hiyo ambapo akizungumza kwa njia ya simu, kamanda wa polisi mkoani Tabora Suzan Kaganda akidhibitisha kutokeaa tukio hilo.

0 comments:

Post a Comment