Wachezaji
wa Simba na Ndanda FC wakiingia Uwanjani wakati wa mchezo wa maalum wa
kusherehekea Ndanda Day uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Nangwanda
Sijaona mjini Mtwara na kudhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya
Jamii (NSSF), kupitia mpango wake wa Wakulima Scheme. Timu hizo zilitoka
suluhu. (Na Mpiga Picha Wetu)
NSSF kupitia mpango wake wa Wakulima
Scheme yadhamini mechi ya kujipima nguvu kati ya Simba ya Dar es Salaam
na Ndanda FC ya Mtwara kwenye uwanja wa CCM wa Nangwanda Sijaona na
kuhudhuriwa na maelfu ya washabiki wa soka mkoani Mtwara.
Mchezo huo pia ulikuwa ni sehemu ya sherehe za Ndanda
Day ulihudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo wa Serikali uliisha
kwa matokeo ya timu hizo kutoka suluhu.
NSSF kupitia mpango maalum wa wakulima schemes wenye
lengo la kuandikisha na kuhudumia wakulima kwenye mfuko ya hifadhi ya
jamii nchini ili kuwawezesha wakulima wote nchini wawe kwenye mfuko wa
huo kupata pensheni ya uzeeni pindi watakapo fikisha umri wa miaka 55
na kuendelea wakulima hao wataweza kulipwa penshion zao hadi watakapo
fariki.
Mpangu huu unamwezesha mkulima kupitia chama cha
wakulima AMCOS kuweza kupata mkopo na taarifa muhimu kuhusu
wakulima,wakulima wanachama wa NSSF wanajiunga bure na kuchangia kuazia
shilingi 20,000 na kuendelea.
Aidha mpangu huu unampa mkulima nafasi pekee ya kulipa
kwa msimu wa mavuno yaani msimu wa mavuno anaweza kulipia kwa mwaka
mzima, miezi anayoweza lipia, lakini pia wakulima wanaweza lipia baada
miezi iliyopitilizia bila malipo msimu wa mavuno.
NSSF likiwa ni shirika pekee lenye kuwapa huduma ya
afya bure wanachama na kuwawezesha wanachama kutoyumba kiuchumi kwa
sababu za gharama za matibabu kwenye familia.
NSSF linawahudumia familia ya mwanachama kwa kuwapa
matibabu bure watoto wanne mwanachama na mwenza.matibabu haya wanapata
pia wakulima wanaojiandikisha kwenye mpango huu wa SHIB wa NSSF na
kuwawezesha kuokoa vipato vyao ambavyo vingetumia kwenye matibabu.
NSSF mkoa wa mtwara unampango wa kuandikisha wanachama
63,000 kutoka kwa wakulima wa vijiji na wilaya zote mkoani mtwara ambazo
ni Tandahimba,Nanyumbu,Masasi ,Nachingwea,Newala,Mtwara Vijijini ambao
wengi ni wakulima wa zao korosho.
Pia kwa akina mama wanapata mafao ya uzazi,kabla na
baada ya kujifungua.aidha wakuliwa wataweza kupata mikopo kupitia SACCOS
zao na kuwawezesha kununua mbolea,madawa ya kuulia
wadudu,pembejeo,dhana mbali mbali za kilimo ili kujiinia kiuchumi
kupitia NSSF SACCOS Loans.
Ofisi ya NSSF Mkoa wa Mtwara umeshatoa jumla ya shilingi
Bilion 1.75 kwa SACCOS zilizokidhi vigezo na kuwainua kimaisha
wajasiriamali, wakulima na wafanyakazi.
Mkuu wa
Mkoa wa Mtwara Kanali mstaafu Joseph Simbakalia akisalimia na timu ya
Ndanda FC kabla ya mchezo wao na timu ya Simba uliofanyika leo kwenye
Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara Kanali mstaafu Joseph Simbakalia akikagua timu ya
Simba wakati wa mchezo wa kirafiki na timu ya Ndanda FC uliofanyika leo
kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Kikosi kamili cha timu ya Simba kilichopambana na Ndanda FC.
Kikosi cha Ndanda FC kikiwa klatika picha ya pamoja kabla ya pambano lao na Simba.
Wachezazaji wa Simba na Ndanda wakichuana katika uwanja wa Nangwanda Sijaona.
0 comments:
Post a Comment