Friday 12 September 2014



KULIKONI Msikiti wa Mtambani Kinondoni? Leo Ijuma mchana msikiti huo maarufu jijini Dar es Salaam, umeungua moto hii ikiwa ni mara ya pili ndani ya siku zisizozidi 40.

Kwa mara ya pili, hitilafu ya umeme inatajwa kama sababu ya kuwaka moto kwa msikiti wa Mtambani.

Mara ya kwanza msikiti huo uliungua gorofa ya pili mwezi uliopita, safari hii umeungua gorofa ya kwanza.

Hata hivyo hakuna mtu aliyepoteza uhai na watoto wote wanaosoma hapo katika shule ya sekondari Mivumoni wamesalimika.

Kutokana na kuchelewa kwa magari ya zima moto, Saluti5 ilishuhudia waumumini wa msikiti huo wakifanya juhudi kubwa za kuzima moto huo kwa kutumia maji ya kawaida.
Wakabeba maji kwenye ndoo kwa hamasa kubwa huku wakisema Allah Akbar (Mungu Mkubwa) hadi kufanikiwa kuuzima moto huo. Wakati magari matatu ya kuzima moto yakiwasili msikitini hapo tayari moto ulikuwa unaelekea kuzimika.


 Harakati za kuzima moto zikiendelea
Harakati za kuzima moto zinaendelea bila kuchoka
Juhudi zinaendelea
Ni mshikamano wa hali ya juu
Hakuna kupumzika mpaka moto uzimike
Hali ilivyokuwa msikiti wa Mtambani Ijumaa mchana
 Hapa sala ya Ijumaa haiwezekani kwa leo hadi moto uzimike
Harakati za kuzima moto zinaendelea bila kuchoka
Shughuli bado pevu
Lango la kuingilia magari likifunguliwa kuruhusu gari la fire liingie
 Gari la zima moto likiingia ndani
Gari la kwanza la zima moto 
Gari la pili la zima moto likielekea Mtambani
Msafara wa magari ya wokozi

0 comments:

Post a Comment