Wednesday 30 July 2014

 

Takribani watu 20 wanadaiwa kupoteza maisha huku wengine wengi wakijeruhiwa baada ya basi la Moro Best lililokuwa linatoka Mpwapwa kwenda Dar es Salaam kugongana uso kwa uso na lori eneo la Pandambili, Kongwa mkoani Dodoma leo. Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali ya Mkoa Dodoma huku wengine wakipelekwa Hospitali ya Mpwapwa.





0 comments:

Post a Comment