Mkoa wa Dodoma unatarajia kuzindua Mradi wa Kuboresha na kuimarisha mfumo wa uuzaji na usambazaji wa dawa katika wilaya zote.
Hatua hiyo inalenga kuboresha
na Kuimarisha Mfumo wa Afya ili kukabiliana na upungufu wa huduma za
dawa katika Hospitali ,Vituo vya Afya na Zahanati katika Mkoa wote wa
Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo
vya habari iliyotolewa leo mjini Dodoma chini ya Mradi wa Tuimarishe
Afya wa Uswis na Tanzania , duka mmoja la dawa litasaidia usambazaji wa
dawa za binadamu inapotokea upungufu katika Bohari Kuu ya Dawa(MSD) .
Taarifa
hiyo imetaja kuwa Duka la hilo ni Bahari la mjini Dodoma ambalo ndio
limechaguliwa baada ya taaratibu za manunuzi kufuatwa , hatimaye kupewa
jukumu usambzaji wa dawa katika Hospitali na Vituo vya Afya ili
kukabiliana na upungufu wa dawa.
Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana
na Mradi wa Kukuza na kuimarisha Mfumo wa Afya (HPSS) umeadhamiria
kukabiliana na tatizo la upatikanaji wa huduma za dawa kwa wananchi kwa
kutafuta duka la dawa litakalosaidia kusambaza na kuuzia wilaya zote
endapo itatokea MSD hawana dawa zinazohitajika.
Taarifa hiyo imesisitiza kuwa
hatua hiyo ni mwanzo wa juhudi mbalimbali za Serikali na wadau wengine
za kukabiliana na upungufu wa dawa katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya
kuboresha afya za wananchi na kuimarisha ustawi wa Taifa kwa ujumla.
Aidha taarifa hiyo imeongeza
kuwa katika makubaliano huo wahudumu watatakiwa kuzingatia taratibu zote
zinazosimamia huduma za uuzaji na usambzaji wa dawa ili kulinda afya za
wananchi.
Uzinduzi wa mpango huo unaratajiwa kufanyika katika Hotel ya Dodoma kesho.
0 comments:
Post a Comment