Afisa
Habari, Elimu na Mawasiliano wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa
Vitendo Tanzania (Law School) Bi. Scholastica Njozi akiwaeleza jambo
waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa ziara iliyofanywa kwenye
Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Habari wa Wizara
ya Katiba na Sheria Bw. Omega Ngole.
Mkuu
wa Kitengo cha Mitihani wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo
Tanzania (Law School) Ipyana Mwaikambo akiwaeleza waandishi wa habari
(Hawapo pichani), Kuhusu idadi ya wanafunzi waliodahiliwa toka Taasisi
hiyo imeanzishwa ambapo alisema zaidi ya wanafunzi 4000 wameshadahiliwa
mpaka sasa, wakati wa ziara iliyofanywa kwenye Taasisi hiyo leo Jijini
Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Taasisi ya
Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) Bi. Scholastica
Njozi.
Muonekano wa ndani wa Chumba cha Mahakama katika Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School)
Serikali yatumia zaidi ya Bilioni 16 kujenga Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo (the law school of Tanzania).
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es
salaam na Msemaji wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Omega Ngole wakati
wa ziara ya waandishi wa habari katika taasisi hiyo iliyolenga kuona
hatua iliyofikiwa tangu kuanza kwa ujenzi wake mwaka 2010.
“Baada ya kukamilika kwa ujenzi
huu mwaka 2013 uendeshaji wa mafunzo ulihama kutoka chuo kikuu cha Dar
es salaam na kuanza kutumika kwa majengo haya ya kisasa yaliyojengwa na
Serikali kupitia Wizara ya Katiba na sheria”
Akifafanua Ngole amesema ujenzi
huo umehusisha ujenzi wa Mahakama ya mafunzo, (Teaching Court) vyumba
vya madarasa (leacture theartres),Maktaba ya Kisasa (Library) Jengo la
Utawala ( Admistration block) Mgahawa na nyumba za watumishi.
Pia Ngole alitoa wito kwa
wanasheria wote wanaohitimu katika Taasisi hiyo kuwa tayari kutoa huduma
popote pale nchini Tanzania kwa kuwa Serikali imetumia fedha nyingi
kuanzisha Taasisi hiyo ili iwanufaishe wananchi wote.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo
cha mitihani bw. Ipyana Mwaikambo alisema Taasisi hiyo imeshadahili
wanafunzi zaidi ya 4000 toka kuanzishwa kwake mwaka 2008 hadi sasa.
Naye Mmoja wa wanafunzi wa Taasisi
hiyo Bw. Edwin Rweykaza amesema Taasisi hiyo inatoa msisitizo katika
mafunzo ya vitendo na kuwajengea uwezo wa kutimiza majukumu yao mara
baada ya kuhitimu.
Kuhusu maadili Rweykaza alibainisha kuwa ni swala linalopewa kipaumbele kwa wanafunzi wote wanaojiunga na Taasisi hiyo.
Serikali imetimiza ndoto ya miaka
mingi ya kujenga majengo ya kisasa ya Taasisi ya Mafunzo ya uanasheria
kwa vitendo Tanzania (The law school of Tanzania) inayotoa mafunzo kwa
vitendo kwa wahitimu wa shahada ya kwanza ya sheria wanaotarajia kufanya
kazi kama mawakili kwa lengo la kuongeza stadi na ujuzi wa wanasheria
hao katika kuwahudumia wananchi.
0 comments:
Post a Comment