Friday 1 August 2014


Kijana mmoja anayekadiliwa kuwa  na umri wa miaka 27aliyefahamika kwa jina la Joseph ponera  ambaye ni mkazi wa   mtaa wa merikebu kata ya bombambili manispaa ya songea amepigwa hadi kupoteeza maisha    na wananchi wenye hasira kali kwa kudaiwa kuwa  ni mwizi wa pikipiki.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Ruvuma mihayo msikhela amesema mnamo majira yaa saa mbili usiku vijana wenye hasira kali walivamia nyumbani kwa kijana huyo na kuvunja mlango wa chumba anacholala na kumpiga kwa kutumia zana mbalimbali kama vile miti na malungu.

ALISEMA " Ninakiri kupokea taarifa za kifo cha Kijana Joseph ponera   katika mtaa wa merikebu kata ya bombambili manispaa ya songea mapema hii leo kupitia kwa viongozi wa merikebu kata ya bombambili manispaa ya songea na mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hosip[iotali ya rufaa ya mkoa wa ruvuma"

Aliendelea kuesema kuwa jeshi hilo bado linaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo  la aina yake kutokea tangu kuanza mwaka huu na kwamba pindi upelelezi utakapokamilika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi wnanchi watakaohusika.

Aidha alisema vitendo vya kujichukulia sheria mkononi si vya kuvumiliwa hata kidogo maana vyombo vya dola ndivyo vyenye jukumu la kutoa hukumu kwa mtu nayebainika kutenda kosa lolote.

kamanda mihayo msikhela ametoa wito kwa jamii kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika mapambano dhidi ya uhalifu na wahalifu ili kuendelea kudumisha usalama kwa nchi.

0 comments:

Post a Comment