Rudisha alikuwa bingwa wa Olimpiki mjini London mwaka 2012
Nigel Amos ana miaka 20
Bingwa
wa Olimpiki na ambaye pia anashikilia rekodi ya dunia katika mbio za
mita 800 mkenya David Rudisha aliambulia medali ya fedhakatika
mashindano ya Jumuiya ya madola.
Hii
ni baada ya kushindwa na mshindani wake wa karibu Nijel Amos mwenye
umri wa miaka 20 katika mashindano hayo yanayoendelea mjini Glasgow
Scotland.
Amos,
ambaye alishinda medali ya fedha katika mashindano ya olimpiki mjini
London alimaliza mbio hizo kwa kishindo baada ya kutoka nyuma ya Rudisha
na kumpiku.
Kwa
kawaida, Rudisha alikuwa mbele wakati wa mbio hizo kwa mita 150 na
kudhibiti mbio zenyewe kama alivyofanya alipovunja rekodi mwaka 2012.
Lakini
alikiri kuwa mbio hizo hazikuwa ngumu , ila mita miamoja za mwisho
ndizo zilizomtatiza na hapo ndipo Amos aliweza kumpiku Rudisha.
Baada
ya kupata jeraha baya la goti mwaka 2013, Rudisha amekuwa mbioni
kuuguza jeraha lake na pia umekuwa wakati mgumu wake kwani washindani
wake wamekuwa pia wakifanya mazoezi wakilenga kumshinda.
Alionekana kuishiwa na nguvu wakati Amos kutoka Botswana alipompiku na kuanza kusherehekea na kushinda dhahabu.
Rudisha
mwenye umri wa miaka 25 alimaliza mbio hizo kwa dakika 1:45.48 nyuma ya
Amos huku Andre Olivier wa Afrika Kusini akinyakua Shaba.
0 comments:
Post a Comment