Pichani
wa pili kulia ni Mchekeshaji Mahiri kutoka nchini Kenya,Anne Kansiime
akifafanua jambo mbele ya Wanahabari kuhusiana na burudani yake kubwa
atakayoinyesha hapo kwesho siku ya Jumamosi kwa mashabiki wake katika
ukumbi wa Golden Tulip,jijini Dar,Kulia kwakwe ni mchekeshaji mwingine
kutoka nchini Kenya,Fred Omondi
Mmoja
wa wachekeshaji mahiri kutoka nchini Tanzania,atambulikae kwa jina la
kisanii Mc Pili Pili akielezea jambo kwenye mkutano wa Wanahabari
uliofanyika mapema leo jijini Dar,wa pili shoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Radio 5, Robert Francis,ambao ndio waandaaji wa Onesho hilo la vichekesho.
Baadhi ya Wanahabari walioshiriki mkutano huo wa wasanii wa vichekesho uliofanyika mapema leo jijini Dar
Mchekeshaji Anne Kansiime anatarajiwa kutoa burudani kubwa siku ya Jumamosi kwa mashabiki wake katika ukumbi wa Golden Tulip.
Akizungumza na
waandishi wa habari katika ukumbi wa Sports Lounge, mkali huyo wa
kuchekesha na sanaa za majukwaani amesema mashabiki wake watarajie mambo
makubwa hapo Jumamosi.
‘Hii
ni mara yangu ya kwanza kuja Tanzania, hivyo mashabiki wangu watarajie
burudani ambayo itaacha mbavu zao hoi, lakini pia watapata nafasi ya
kujifunza vitu vingi kupitia vichekesho vyangu’ alisema Anne.
Kwa
upande wake, mchekeshaji mwingine kutoka Kenya atayetoa burudani, Fred
Omondi, amesema watanzania watarajie burudani kali kama lilivyo jina la
burudani yenyewe, Cheka Kwa Nguvu.
‘Usiku
wa Jumamosi utawakutanisha moja ya wachekeshaji mahiri barani Afrika,
hivyo watanzania waje kwa wingi kushuhudia burudani hii’ alisema Fred.
Naye mchekeshaji
Pilipili kutoka Tanzania amesema usiku wa leo utakuwa usiku
wa kukumbukwa hasa kwa vichekesho alivyowaandalia mashabiki wake.Usiku wa Cheka Kwa Nguvu unaandaliwa na kituo cha Radio 5 na pia utaambatana na burudani ya muziki kutoka ODAMA Band.
Akizungumzia tukio
hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Radio 5, Robert Francis
amewataka wapenzi wa burudani ya vichekesho kuhudhuria kwa wingi ili
wafurahie burudani waliyowaandalia. ‘Usiku huo utakuwa ni
maalumu kwa watanzania kufurahia Utanzania wao, kwani kucheka ni
sehemu muhimu kwa maisha ya mwanadamu’ alisema Robert.
Kansiime amejipatia
umaarufu kupitia mitandao ya kijamiii ambako alianza kwa kuweka vipande
vya video akiigiza kama mwanamke wa kiafrika anayekutana na
changamoto mbalimbali za maisha.
Mchekeshaji huyo
wa kike, ambaye pia huendesha kipindi cha “Don’t Mess With Kansiime”
kwenye kituo cha Citizen TV, anatajwa kuwa mwanamke mwenye kipaji cha
pekee nchini Uganda na Afrika Mashariki kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment