Sunday, 17 August 2014




Jeshi la Polisi mkoani Mtwara limefanikiwa kuokota milipuko 10 iliyotengenezwa kienyeji ambayo ilikuwa imetelekezwa jirani na Shule ya Msingi Raha Leo na Sekondari ya Raha Leo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Augustino Ollomi alieleza kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 11 na kwamba waliweza kuibaini milipuko hiyo baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema.
Alisema kuwa baada ya polisi kupata taarifa, ilichukua hatua za haraka ikiwa ni pamoja na kufika eneo la tukio na kufanikiwa kuokota milipuko kumi iliyotengenezwa kienyeji.
Kamanda Ollomi alibainisha kuwa mabomu hayo yalitengenezwa kwa kutumia chupa za plastiki zenye ujazo wa nusu lita zilikuwa zimejazwa mbolea ya urea, iliyochanganywa na mafuta ya taa huku zikiwa zimefungwa pamoja na urojo wa baruti, waya wa kulipua na chuma cha kulipua zipatazo saba zikiwa zimefichwa kichakani jirani na zilipo shule.

0 comments:

Post a Comment