Iringa, mkoa ambao ulishika nafasi ya tatu kitaifa
katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2013, yapo mambo
kadhaa ya kusikitisha na ya kushangaza ambayo pengine hayapaswi kupewa
nafasi katika mitihani ijayo mkoani humo.
Moja ya mambo hayo ni wanafunzi wanne katika Shule
ya Msingi ya Mkombilenga iliyoko katika Halmashauri ya Wilaya ya
Iringa, ambao hawakufanya mtihani huo siyo kutokana na kutokuwa na sifa,
bali inaelezwa kuwa waliwakimbia polisi waliokuwa wakilinda kituo
hicho.
Wanafunzi hao wanne wamo katika kundi la watoro
ambao ni sehemu ya wanafunzi 226 ambao hawakufanya mtihani wa kuhitimu
elimu ya msingi mkoani humo mwaka jana.
Kati yao, wanafunzi 196 hawakufanya mitihani
kutokana na utoro, 12 kutokana na vifo, 13 kutokana na kuwa wagonjwa na
watano walipata ujauzito wakiwa shuleni.
Lakini ukweli kuhusu polisi ni kwamba Kuwapo kwa polisi katika vituo vya mitihani ya kitaifa, hasa ya darasa la saba ni jambo ambalo limezoeleka.
Kazi ya askari hawa huwa ni kulinda usalama kwa
watahiniwa na wasimamizi, lakini zaidi usalama wa mitihani yenyewe,
kabla na baada ya kufanyika kwake.
Pia polisi huwa na wajibu wa kuchukua hatua dhidi
ya wale ambao hubainika kufanya au kusaidia kufanyika kwa udanganyifu
kwenye mitihani.
Kwa mujibu wa taratibu zilizopo, wanafunzi hupewa
maelezo kuhusu mchakato wa mitihani, ambayo kufanyika kwake
huwashirikisha wageni ambao ni wasimamizi kutoka nje ya shule wanazosoma
wanafunzi hao na polisi ambao huwa ni walinzi wa amani.
Hata hivyo, katika baadhi ya maeneo inawezekana
somo hili huwa halipewi uzito stahili au halizingatiwi ipasavyo kwa
wanafunzi ambao huwa katika matarajio ya kufanya mitihani.
Kisa cha Iringa
0 comments:
Post a Comment