Kanda ya Nyanda za Juu Kusini imetakiwa kuongeza tija katika sekta ya kilimo ili kiweze kuwa na mafanikio endelevu.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mizengo Panda alipokuwa akifungua maonesho ya Nanenane Kanda ya Nyanda
za Juu Kusini baada ya kukagua mabanda hayo jijini Mbeya.
Waziri
Pinda amesema kuwa katika kanda hiyo mambo mengi yameboreshwa sana
katika mabanda ya maonesho ikilinganishwa na misimu iliyopita. Amesema
kuwa katika kilimo cha zao la mahindi, kanda hiyo imeongeza thamani
katika vifungashio. Amesema pamoja na hilo bado juhudi zinahitajika
katika kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao mengi zaidi. Amesema
kuwa kilimo cha mazao ya chakula kina umuhimu mkubwa katika kanda hiyo
hasa msingi wake ukijengwa katika lishe.
Aidha,
Waziri Mkuu amesisitiza kilimo na ufugaji kibiashara ili kiweze kutoa
mafanikio chanya. Amewataka kuwashirikisha vijana katika kilimo na
ufugaji kibiashara ili mafanikio yao yaweze kuwavuta vijana wengine
kushiriki katika kilimo na ufugaji.
Waziri
Mkuu ameshauri kuwa viongozi wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wafikirie
kuipanga mikoa yao kulingana na aina kuu mazao yanayolimwa katika mikoa
yao.
Waziri
Pinda amepongeza kilimo cha mahindi katika ukanda huu. Amesema kuwa
mahindi ni zao linalolimwa kwa asilimia 45 ya mazao yote yakilimwa na
asilimia 65 ya kaya nchini. Amesema kuwa soko la zao la mahindi ni kubwa
ndani na nje ya nchi. Amefarijika na kuwepo kwa baadhi ya makampuni
yanayosindika zao la mahindi na kubainisha changamoto kubwa ni tija kuwa
chini sana. "Afrika na Duniani Tanzania ni ya mwisho katika tija kwenye
zao la mahindi" aliongea kwa uchungu Waziri Mkuu.
Warizi
Mkuu amesisitiza matumizi ya mbolea katika kilimo. Amesema kuwa mbolea
ni muhumu sana katika kilimo nchini na kuwataka wananchi kuachana na
dhana kuwa mbolea haina muhimu katika kilimo na inaharibu udongo.
Amesema kuwa umuhimu wa mbolea katika udongo unabaki palepale isipokuwa
matumizi ya mbolea hutofautiana kutokana na mahitaji ya udongo.
Akiongelea
matumizi ya mbegu bora, waziri mkuu amesema kuwa mbegu bora ni muhimu
sana kuleta tija katika sekta ya kilimo nchini. Amesema kuwa Tanzania
ina kiwango cha chini sana cha matumizi ya mbegu bora. Amesema
kuwamatumizi ya mbegu bora ni asilimia 10 tu.
Maadhimisho
ya 22 ya Nanenane yanaongozwa na kaulimbiu isemayo "matokeo makubwa
sasa, kilimo ni biashara" yataendelea hadi kilele chake tarehe 8/8/2014.
Katika
salamu za Katibu Mkuu wa TASO Nyanda za Juu Kusini, Ramadhani Kiboko
amesema kuwa nyanda hiyo imejipanga kuongeza matumizi sahihi ya
teknolojia. Amesema kuwa maadhimisho ya Nanenane yamekuwa yakitumika
kama shamba darasa kwa watu wote kwenda kujifunza mbinu mbalimbali za
kimkakati katika kuboresha kilimo nchini.
Akiongelea
nafasi ya katiba mpya amesema kuwa yamewasilishwa maoni kuwa katiba
mpya iondoe migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji na kuweka
uwiano wao nchini.
0 comments:
Post a Comment