Mtangazani
Mahiri wa Redio 88.5 Clouds FM kupitia kipindi cha Jahazi, Ephrahim
Kibonde akipingana na Askari wa Usalama barabarani wakati alipotakiwa
kutii sheria bila shurti,mapema asubuhi hii jijini Dar es salaam.
Kibonde
anadaiwa kusababisha ajali asubuhi hii eneo la Makumbusho, ikiwa gari
aliyokuwa akiendesha kuigonga gari ya dereva mwingine kwa nyuma. Trafiki
walifika eneo la tukio na kupima ajali, Kibonde alipoona hivyo akarudi
nyuma na kuendesha gari lake kuondoka eneo la tukio bila kufuata
taratibu za usalama barabarani,hali iliyomlazimu yule Trafiki kutumia
gari lililogongwa kumfukuzia.
Walifanikiwa
kumkamata eneo la Mwenge na Trafiki aliingia katika gari lake na
kumwomba arudi eneo la ajali ili wakapime na kuchora mchoro wa ajali.
Kibonde aligoma na kumtaka trafiki ashuke katika gari lake,Trafiki naye
hakutana kufanyi kwa maana ya kuwa aligoma kushuka na kumuamuru Kibonde
arudi eneo la tukio.
Kibonde
aliondoa gari na kuendelea na safari yake huku yule Trafiki akiwa ndani
ya gari hiyo, Trafiki aliwasiliana na wenzake ambao walianza kuifuatilia
gari hiyo ya Kibonde kama walivyopewa maelekezo na mwenzao aliopo ndani
ya Gari hiyo.
Mara
Kibonde akatokea maeneo ya mataa ya Ubungo, hapo kulikuwa na Trafiki
mwingine aliyekua eneo hilo akaipiga mkono gari ya Kibonde na ambapo
inasemekekana hakusimama na badala yake ikaja gari nyingine na
kuichomekea kwa mbele na hapo ndipo alipotiwa mbaroni! Aligoma
kuendesha gari ikabidi livutwe hadi polisi Urafiki na yeye kuwekwa chini
ya ulinzi na baadae akahamishiwa Kituo cha Oystabay ambako yupo mpaka
sasa.
Inadaiwa kuwa Kibonde alikuwa amelewa sana,hali iliyopelekea kufanya hayo yote ikiwa ni pamoja na kuwajibu vibaya Askari hao.
0 comments:
Post a Comment