Mtuhumiwa Abdul Ghan Peer Bux.
Wapakistani
wawili, Abdul Ghan Peer Bux na Shahbaz Malk (pichani) waliokamatwa
wakiwa na Watanzania wanaotuhumiwa kwa kukutwa na madawa ya kulevya
wametoroka nchini.
Watuhumiwa
hao walikamatwa Februari 21, 2011wakiwa na madawa ya kulevya yenye
thamani ya shilingi bilioni 6.2, Mbezi Beach maeneo ya Jogoo
jijini Dar sa Salaam.Habari
za uchunguzi ndani ya Mahakama Kuu zinasema kuwa, Jaji Grace
Mwakipesile anayesikiliza kesi hiyo inayotarajiwa kuendelea
kusikilizwa kesho Jumatano, ametoa amri ya kukamatwa kwa watuhumiwa
hao.
Kesi
hiyo ambayo ilisikilizwa mahakamani hapo Julai 4, mwaka huu ilidaiwa
kuwa Wapakistani hao walikamatwa na kikosi kazi cha kuzuia na
kupambana na madawa ya kulevya kisha kudhaminiwa lakini wametoweka bila
kuhudhuria mahakamani hata siku moja.
Mtuhumiwa Shahbaz Malk.
Imeelezwa
kuwa, baada ya watuhumiwa hao kudhaminiwa na wadhimini wawili, Julai 4,
mwaka mahakama iliambiwa kuwa wadhamini hao wamefariki dunia. Hata
hivyo, jaji anayesikiliza kesi hiyo aliwaagiza ndugu waliotoa taarifa
hiyo kupeleka cheti halisi cha kifo kesho na watuhumiwa wahudhurie
mahakamani hapo.
Madawa ya kulevya yaliyokamatwa na watuhumiwa hao yenye thamani ya shilingi bilioni 6.2.
Watanzania
waliokamatwa na Wapakistani hao waliachiwa huru baada ya kulipa dhamana
ya shilingi 10,000,000 ambapo wadhamini wao ni Raza Hussein Kanji
ambaye alipewa stakabadhi namba 3406367 na Nazar Mohamed Nurd alikatiwa
yenye namba 3406355.
Kamanda wa Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya nchini, Godfrey Nzowa.
Februari
21, 2011 polisi chini ya kamanda wao, Godfrey Nzowa waliwakamata
Wapakistani hao wakiwa na Watanzania wawili, William Chonde na Kambi
Zuberi ambao wapo nje kwa dhamana wakituhumiwa kukutwa na madawa ya
kulevya yenye thamani ya shilingi bilioni 6.2.
0 comments:
Post a Comment