Saturday 16 August 2014

 Jamani imeniuma mnoooo..... yaani baba mzazi umpige Malaika kama huyu hadi umtoe Roho????? kakosa nini hasa kiasi cha kustahili adhabu hiyo?????
Inasemekana kuwa huyu mtoto ameuliwa na baba yake mzazi kwa kipigo kikali...maeneo ya Moshi Vijijini- kijiji cha Mero...Yaani ukiangalia Hata picha zake zinaonyesha kabisa jinsi mwili wa huyu mtoto Malaika ulivyojaa makovu ambayo ni ya kipigo cha mara kwa mara.....Yesu turehemu...
Inasemekana mtoto anakaa na baba yake mzazi na mama wa kambo... Ebu angalia jinsi huyu mtoto alivyoumizwa jamani..... yaani nimelia kwa uchungu maana huyu mtoto ameteseka sana kufa 


kwake.....alitamani mtu aje amkamate baba yake ili asiendelee kumpiga lakini hakutokea....alilia sana ili baba amuache lakini bado akaendelea kupigwa sana.... aliona jinsi baba anavyomuonea kwa kuwa yeye sii mkubwa kama baba yake hata ajitetee kwa kumzuia (mfano watu wazima wanavyopambana)
 Mwili wa mtoto umeviria damu kwa kipigo toka kwa baba yake mzazi ambae taarifa zinasema kuwa anaitwa  Morsi Clemence, na mara nyingi shughuli zake ni vibarua vya hapa na pale...... Natamani sana kufanya kampeni maalumu ya ''OKOA MTOTO'' ili jamii iwalinde watoto wetu...
Tukio hili limetokea eneo linaloitwa kitu kama kwa ''Raria'' ambapo ni katikati ya njia panda na kabla hujafika Moshi mjini.... jamani huyu baba naskia amekimbia baada ya kujikuta ameua mwanae kwa kipigo kizito... Marehemu kazikwa jana baada ya babu mtoto kusema azikwe wakati baba mtoto (mtuhumiwa) akitafutwa popote alipo....
Mbaya zaidi nimeambiwa kwamba huyu baba ana mke ambae ni mama wa kambo na huyu mtoto ambae ndiye aliyekamatwa baada ya mume wake kukimbia kusikojulikana.... BINAFSI NINA MASWALI MENGI BAADA YA KUSIKIA KUNA MAMA AMBAE ANAISHI NA HUYU BABA ALIYEUA.... MBONA MTOTO ANA MAKOVU MENGI KIASI HIKI??? KWANI HUYO MAMA HAKUWA ANAMTETEA HUYU MTOTO WAKATI ANAPIGWA NA BABAKE???? IMENIUMA SANA SANA LAKINI NDO HIVYO.

0 comments:

Post a Comment