Ripoti za hivi karibuni
zinaarifu kuwa shambulizi la angani la Israel limewauwa watu saba katika
shule moja ya umoja wa mataifa katika mji wa Rafah.
Walioshuhudia wanasema kuwa kombora hilo lilipiga eneo moja karibu na mlango wa shule hiyo.Msemaji wa Jeshi la Israel Luteni kanali Peter Lerner amesema kuwa baadhi ya wanajeshi wanaondolewa katika eneo la Gaza ,lakini oparesheni hiyo itaendelea.
Wajumbe wa Hamas wamewasili katika mji mkuu wa cairo nchini Misri kwa mazungumzo ya kusitisha vita.
Israel imesema kuwa haipelekwa wawakilishi wake.
Wakati huohuo Msemaji wa umoja wa mataifa katika eneo la Gaza ameonya kuwa maafa makubwa ya kiafya huenda yakazuka katika eneo la Gaza kufuatia wiki tatu za mapigano katika eneo hilo.
Chris Gunness kutoka shirika la umoja wa mataifa linalosimamia misaada amesema kuwa maafisa wa afya katika eneo la Gaza wanaendelea kulemewa.
Amesema kuwa hospitali,zahanati na ambulansi zimeharibiwa na kwamba zile zinazotoa huduma zimezidiwa huku asilimia 40 ya maafisa wa afya wakishindwa kufika kazini.
0 comments:
Post a Comment