BAADA
ya timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya miaka 17, Serengeti
Boys kutolewa katika michezo ya kuwania kufuzu fainali za Afrika za
vijana na Afrika kusini kwa wastani wa mabao 4-0, Rais wa shirikisho la
soka Tanzania, TFF, Jamal Emil Malinzi amekiri kuwa bado timu
haijaandaliwa vizuriRais
Malinzi amesema tatizo la timu ni maandalizi yasiyoridhisha
yanayochangiwa na kukosa mfumo sahihi na mpango mzuri wa soka la vijana.
“Tatizo
letu ni lile lile, kwenye maandalizi, lakini tunapozungumzia maandalizi
tunazungumzia uwezo wa kiuchumi, kwamba timu yetu inaandaliwaje,”
Alisema Malinzi.
“Tunaweza
kusema timu imejitahidi, Lakini kiukweli hii ndio mechi yao ya pili ya
kimataifa, mechi yao ya kwanza walicheza na Afrika kusini nyumbani,
“
Kwahiyo lazima sisi tukae kama nchi, kama shirikisho ili tuweze
kuangalia programu zetu za soka la vijana ili watoto kama hawa kabla
hawajaingia katika mechi kama hizi wawe wameshakaa kama timu kuanzia
umri wa 12, 13, 14 na 15 yaani wakae miaka minne kwenye timu ya
taifa,” Aliongeza Malinzi.
Aidha, Rais Malinzi alisema shirikisho hilo limejipanga upya ili kuhakikisha nchi inakuwa na mfumo sahihi wa soka la vijana.
“Kipo
ambacho kinafanyika, tunaandaa mpango wa kitaifa wa maendeleo ya soka
la vijana na tutazindua mwezi wa 10 mwaka huu, siku ambayo TFF itatimiza
miaka 10 ya kujiunga na FIFA na tutaeleza haya tunayoyasema ili kama
nchi tuwe na mpango endelevu wa soka la vijana,”
0 comments:
Post a Comment