MAMLAKA ya
maji safi na Maji Taka mkoa wa Mbeya imewanasa wakandarasi wawili wanaojenga jengo
la ghorofa 5 lililopo Kitalu D barabara ya Lupa jijini Mbeya kwa kutumia maji
bure bila Mita.
Hatua ya
kukamatwa kwa watuhumiwa hao ambao ni wakandarasi na wasimamizi wasaidizi wa jingo
hilo imekuja baada ya ukaguzi unaondelea kufanywa na mamlaka hiyo juu ya
matumizi halali ya Maji kwa watumiaji.
Akizungumza
kukamatwa kwa Wakandarasi hao Mwanasheria wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka
mkoa wa Mbeya, Simon Bukuku alisema kuwa mnamo majira ya jioni katikati ya Jiji
la Mbeya waliwanasa wakandarasi hao wakitumia maji bila kutumia mita ya
Mamlaka.
Bukuku
alisema kuwa hadi sasa hawajajua hasara iliyotokana na matumizi hayo ya maji
kwa kuwa wamekuwa wakitumia maji hayo kwa muda mrefu tangu waanze ujenzi huo.
‘’Tutatoa
taarifa za hasara iliyotokana na matumizi hayo ya maji baada ya tathmini hapo
kesho,’’alisema Bukuku.
Alisema kuwa
baada ya kubaini matumizi hayo ambayo ni kinyume cha sheria za matumizi ya maji
waliwasiliana na vyombo vya usalama ambapo kwa msaada wa askari polisi
wanaofanya doria ya Pikipiki wakawanasa watuhumiwa wawili ambao ni Bryson
Mwasile na Emmanuel Mwakipesile.
Alibainisha
kuwa baada ya kuwakamata wamefunguliwa kesi katika kituo cha Polisi cha Kati
Jijini Mbeya kwa namba MB/IR/6563 na kwamba nyumba hiyo ambayo inaelezwa
mmiliki wake kuwa ni Kanji Lalji iko katika ujenzi kwa muda mrefu.
Bukuku
alisema kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa wakifanya makosa kinyume na sheria za
maji na usafi wa mazingira ya mwaka 2009, kifungu cha 47 na 50.
Pia alisema
kuwa makosa hayo yamao katika sheria za makosa ya Uhujumu wa Uchumi chini ya
sheria za Usalama wa Taifa Cap 47, kifungu cha 3(b) na Cap 3(d) ambapo
watuhumiwa ambao wanashikiliwa na polisi watafikishwa mahakamani kesho asubuhi.
|
0 comments:
Post a Comment