Wednesday 23 July 2014

tweet 2Unaambiwa facebook imebaki kuwa mtandao wa kijamii unaotumiwa sana na wakenya takriban million 3.8 wenye account za mtandao huu ambapo ripoti mpya inaonyesha mtandao wa linkedin ni wa pili ukiwa na watu milioni 1 huku twitter ikishikilia nafasi ya tatu kwa kusajili watumiaji takriban laki sita na nusu.
Digital Rand watafiti na watoaji wa ripoti hiyo pia wanasema utumiaji wa Twitter uliiongezeka kati ya mwaka 2012 na 2013 ambapo MKenya wa kwanza kujisajili twitter ni @kamuiri na ilikua March 28 2007 akifatiwa na @kenyamoto pamoja na @Sonnimuriuki.
Kwenye sentensi nyingine ni kwamba watu milioni 4 hutumia facebook kila siku kwenye shughuli zao huku ripoti ikionyesha pia kwamba Wakenya walioko Twitter wanaushawishi wa  followers 120,199,588 kwa ujumla na wanaowafollow ni 49,539,705 kwa ujumla na Mkenya wa wastani anafollow watu 89 huku followers wake wakiwa ni 214″
tweet 3Pamoja na hiyo rekodi, unaambiwa asilimia 19 ya wakenya hawajawahi kutweet mwaka huu wa 2014 ambapo asilimia 65 ya twitter accounts zote hazitumiwi.
Ripoti hii inatokea wakati ongezeko la matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii yanayozua mgawanyiko na uchochezi kwa wananchi yanazidi kuripotiwa ambapo ofisi ya kiongozi wa mashtaka upande wa serikali inaandaa muswada wa kudhibiti uhalifu wa mtandao [Cyber Crime and Computer Related Bill]
Wakaazi wa jiji la Nairobi wanachangia asilimia 74 ya Wakenya wote twitter huku asilimia 11 ya Wakenya wa twitter wakiwa  nje ya nchi ambapo kwenye hesabu, inaonekana kuna tweets milioni 300 zimetumwa na Wakenya mbalimbali mpaka sasa.

0 comments:

Post a Comment