WATAALAMU wa masuala ya lishe wamesisitiza mtoto anapaswa kunyonyeshwa kwa dakika 45 bila kukatishwa.
Hata
hivyo, imeelezwa kutokana na teknolojia za kisasa, akina mama wengi
wanakiuka ushauri huo wa kitaalamu kutokana na baadhi yao kutumia muda
mwingi kwa shughuli nyingine ikiwemo matumizi ya simu za mkononi.
“Kazi
ya kumnyonyesha mtoto inatakiwa kufanywa kwa dakika 45, bila kumkatisha
mtoto, lakini hizi teknolojia zetu zinafanya wazazi watumie muda mwingi
na simu au shughuli zingine jambo ambalo si sahihi,” alisema Daktari
Bingwa wa Watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Augustine Massawe.
Aliyaeleza
hayo juzi jijini Dar es Salaam kwenye mafunzo ya waandishi wa habari
katika kuadhimisha Wiki ya Unyonyeshaji Maziwa ya Mama.
Dk Massawe aliwataka kina mama kuacha kupokea simu wakati wa kunyonyesha watoto ili kuwawezesha kunyonya ipasavyo.
Alisema
matumizi ya simu ni miongoni mwa mambo yanayomvuruga mtoto wakati wa
kunyonya na hasa mama anapozungumza nayo muda mrefu.
Ofisa
katika Kituo cha Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Luitfrid Nnallu
alisema tatizo la utapiamlo limeongezeka hadi kufikia asilimia 42
miongoni mwa sababu ikiwa ni ukosefu wa ujuzi wa unyonyeshaji.
Alisema tatizo ni kubwa kwa zaidi ya asilimia 50 kwenye mikoa ya Dodoma, Lindi, Rukwa na Iringa.
“
Utapiamlo ni tatizo ambalo linachangiwa na mambo matatu, matunzo ya
mtoto, afya na lishe ambayo inaanza tangu unyonyeshaji hadi mtoto kuanza
kupewa vyakula vya nyongeza,” alisema.
0 comments:
Post a Comment