Sunday 31 August 2014

kihesa_0774d.jpg
Mkazi wa Kihesa katika Manispaa ya Iringa, Peter Kalawa akiuliza swali katika mkutano wa hadhara wa Kampeni ya Kituo cha Sheria na haki za Binadamu (LHRC) ya kusambaza uelewa juu ya Katiba kwa wananchi uliyofanyika Kihesa Sokoni hivi karibuni. Wakati wa mkutano CD za sauti ambako Rasimu ya Pili ya Katiba imerekodiwa yote kwa lugha nyepesi, "flash disk" kwa ajili ya madereva wa Bodaboda na machapisho kwa lugha nyepesi vilitolewa bure .
baadhi_b3eab.jpg
Wakazi wa Kihesa katika Manispaa ya Iringa, wakifuatilia kwa umakini mkutano wa hadhara wa Kampeni ya Kituo cha Sheria na haki za Binadamu (LHRC) ya kusambaza uelewa juu ya Katiba kwa wananchi unaendelea katika mikoa 20 ya Tanzania bara na visiwani, uliyofanyika Kihesa Sokoni hivi karibuni.
WAKILI_8a589.jpg



Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Hussein Ngaga.

OFISA ushirika wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Raphael Luvanda ameonja joto ya jiwe baada ya Wanachama wa chama cha kuweka na kukopa, Mbinga Lutheran SACCOS kumjia juu na kumweleza kwamba hawana imani naye katika utendaji wa kazi zake hivyo hawamtaki kumuona akifanya kazi za ukaguzi katika umoja huo.
Sambamba na hilo wanachama hao ambao walionekana kukerwa na tabia za Ofisa ushirika huyo walisema, sababu zao za msingi za kumkataa wamekuwa wakimtuhumu kwa muda mrefu kwamba anafanya kazi zake kwa mrengo wa kushoto na sio kwa maslahi ya wanachama.
Walieleza kuwa bodi husika itazifikisha tuhuma husika kwa mwajiri wake ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo, ili ziweze kufanyiwa kazi huku wakitaka kuanzia sasa shughuli za ukaguzi zifanywe na ofisa ushirika mwingine na sio vinginevyo.

Hali hiyo ilijitokeza katika mkutano mkuu wa wanachama hao uliofanyika juzi mjini hapa, kwenye ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Walisema katika hali ya kusikitisha Luvanda amekuwa na tabia za ajabu hataki kufuata taratibu zake za kazi, badala yake amekuwa mtu wa kupenda kuzua migogoro ya hapa na pale kati ya uongozi wa SACCOS hiyo na wanachama kwa ujumla.
Vilevile katika taarifa yake ya ukaguzi ya mwaka 2013 alishindwa kubainisha wizi wa fedha uliofanywa na aliyekuwa mhasibu wa ushirika huo, Ansilla Kapinga na kusababisha uongozi husika kutumia gharama kubwa kuleta wakaguzi wengine kutoka nje ya wilaya ya Mbinga.
Waliongeza kuwa alifikia hatua, vitabu na nyaraka muhimu za umoja huo alizizuia ofisini kwake akitaa kuzirejesha jambo ambalo lilikuwa likizua malalamiko ya hapa na pale miongoni mwa wanachama na kufanya wakose imani naye.
“Kwa mwenendo huu hatutaweza kuvumilia suala hili, ni vyema ofisa ushirika huyu afanye kazi zake kwa kufuata taratibu zilizowekwa na sio kujenga mipasuko ambayo inavuruga ushirika wetu”, walisema.
Walifafanua kuwa wanazo taarifa kwamba, Luvanda amekuwa hata akitoa taarifa za upotoshaji kwenye maeneo mengine ya mashirika ambayo yanatoa mikopo hapa wilayani, kwa lengo la kugonganisha viongozi husika na wanachama kwa maslahi yake binafsi.
Hata hivyo kwa upande wake Ofisa ushirika huyo alipopewa nafasi ya kujieleza aliishia kwa kuwaomba radhi wanachama hao, na kuondoka bila kutolea maelezo yakinifu yenye kufikia muafaka wa tuhuma ambazo alinyoshewa kidole.


Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG), Mhe. Anna Abdallah akifungua Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
Katibu wa Umoja wa Wanawake Wabunge Tanzania (TWPG), Mhe. Angellah Kairuki (MB) akizungumzia masuala mbalimbali ya kijinsia katika Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Bi. Usu Mallya akitoa mada kuhusiana na suala la kijinsia katika Katiba, wakati wa Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Profesa Ruth Meena akitoa mada juu ya masuala muhimu ya Jinsia ya kuzingatiwa katika Katiba Mpya wakati wa Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Bi. Stella Gailos akitoa mada akitoa mada juu ya masuala muhimu ya Jinsia ya kuzingatiwa katika Katiba Mpya wakati wa Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akifafanua juu ya masuala mbalimbali ya kijinsia wakati Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba akichangia mada wakati Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Hamad Rashid akifafanua jambo wakati Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Fami Dovutwa akifafanua jambo wakati Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba wa Kundi la 201 upande wa Wakulima, Mhe. Agnes Senyagwa akizungumzia kuhusu utoaji elimu kwaajili ya kuongeza nafasi za uwakilishi wa wanawake katika ngazi mbalimbali maeneo ya vijijini, wakati Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Faustina Urassa akifafanua jambo wakati Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakifuatilia Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakifuatilia Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
Viongozi wa Meza Kuu wakiiimba kwa pamoja wimbo wa kuhamasisha wanawake kupigania haki zao wakati wa Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
Wajumbe wakiiimba kwa pamoja wimbo wa kuhamasisha wanawake kupigania haki zao wakati wa Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (MB) akitoa neno la sukrani kwa watoa mada na wajumbe wa Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG), Mhe. Anna Abdallah (kulia) akifanya mahojiano na Mwandishi wa Habari wa Shirika la Habari Tanzania (TBC) mara baada ya kumalizika kwa na Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
Picha ya pamoja ya baadhi ya Wajumbe wa Semina hiyo iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma

 Wadau wa TMT wakiwa kwenye Red Carpet ndani ya Ukumbi wa Mlimani City katika FAinali ya Shindano la Kusaka Vipaji vya Uigizaji lijulikanalo Kama Tanzania Movie Talents (TMT) ambapo  Mshindi wa Shilingi Milioni 50 za Kitanzania Alipatikana
 Ceaser Daniel akiwa na Jaji wa Tanzania Movie Talents (TMT) Single Mtambalike


 Kikundi Cha TMT Survivor kikitoa Burudani
 Kumi Bora ya washiriki Wakiwa katika Picha ya Pamoja na Mkuru
Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Bw Johnson Lukaza akiwa na Mkewe Marian Johnson katika Dhuria Jekundu usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Mlimani City Ambapo Fainali ya Shindano la TMT lilipofanyika na Mshindi Kupatikana.
 Aliyekuwa Mshiriki wa TMT na kufanikiwa kuingia hatua ya ishirini Bora na hatimaye kutolewa kwa Uchache wa Kura, Shiraz Ngasa akiwa katika picha ya Pamoja na Jaji Vyonne Cherrie au Monalisa katika Dhuria Jekundu
Majaji Wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Wakijadiliana jambo kabla ya Mtanange Wa TMT uliokuwa ukirushwa live kupitia Kituo Cha ITV kuanza


Msanii wa muziki Florah Mbasha, Baada ya kufunguka mengi kuhusiana na matatizo katika ndoa yake wiki hii, ameweka wazi kuwa shughuli zake za muziki bado zinaendelea huku akiwa na albam mpya kabisa kwaajili ya wapenzi wa sanaa yake.

Frorah Mbasha amesema kuwa, anamshukuru Mungu kwa kufanikisha kutoa albam mpya inayokwenda kwa jina Nipe Nguvu ya Kushinda, kazi ambayo tayari jamii imeipokea vizuri.

Msanii huyu ambaye amezoeleka kufanya kazi ya muziki pamoja na mumewe Emmanuel Mbasha, amewatoa wasiwasi mashabiki kuwa licha ya mgogoro, Mumewe yupo katika kazi hii.


BARAZA la Mitihani la Taifa (NECTA), limetangaza mfumo mpya wa upangaji wa madaraja ya ufaulu kwa kutumia wastani wa pointi (GPA) ambao utaanza kutumika katika mtihani wa kidato cha nne 2014 na cha sita 2015.

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Charles Msonde, alisema kuwa mfumo huo umekuwa ukitumika katika kupanga madaraja ya ufaulu katika baadhi ya mitihani inayosimamiwa na baraza hilo.

Alisema manufaa yake ni kuwa na mfumo wa kutunuku matokeo wa ina moja katika ngazi zote za mafunzo kuanzia elimu ya msingi hadi elimu ya juu; matokeo yaliyo katika mfumo huo kwenye cheti yatarahisisha kazi ya udahili wa watahiniwa unaofanywa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) na NACTE katika ngazi za juu za mafunzo.

Pia aliongeza kuwa mfumo wa GPA ni rahisi kuelewa kwa wadau wa kada mbalimbali kwa sababu hutoa tafsiri yenye kuonesha mtahiniwa aliye na GPA kubwa ndiye aliye na maokeo mazuri.

Kwa mujibu wa Dk. Msonde, madaraja katika mfumo wa GPA hupangwa katika utaratibu wa Distinction, Merit, Credit na Pass ambapo daraja la juu ufaulu ni Distinction na la chini ni Pass.

Kulingana na utaraibu huo, daraja la Distinction litakuwa na alama kati ya 3.6-5.0, Merit 2.6.3.5,Credit 1.6-2.5, Pass 0.3-1.5 na Fail 0.0-0.2 kwa matokeo ya kidato cha nne wakati wa kidato cha sita Distinction ni kati ya 3.7-5.0, Merit 3.0-3.6, Credit 1.7-2.9, Pass 0.7-1.6 na Fail 0.0-0.6.

“Ukokotoaji wa wastani wa pointi (GPA) ya mtahiniwa hufanywa kwa kuzingatia masomo ambayo mtahiniwa amefaulu. GPA anayopata mtahiniwa wa mtihani wa kidato cha nne hutokana na wastani wa pointi alizopata katika masomo saba aliyofaulu vizuri wakati kwa kidato cha sita ni masomo matatu,”alisema.


Jengo lililolipuliwa.
Mlipuko umeharibu jengo moja la ghorofa 4 kazkazini mashariki mwa Paris na kumuua mvulana mmoja huku watu kadhaa wakiwa hawajulikani walipo.Watano kati ya wale waliotoweka wanadaiwa kuwa watoto.Afisa mmoja wa huduma ya zima moto katika mji huo mkuu amesema haijulikani ni nini kilichosababisha mlipuko huo.
Msemaji huyo amesema kuwa maafisa wa matibabu wamepelekwa katika eneo hilo.