Jumla ya Risasi 295 za Bastola ( Pistol)
, marisau 112 ya bunduki ya Shortgun ( Gobore) aliyokutwa nazo Mansour
Yussuf Himid aliposachiwa nyumbani kwake
Bastola na aina ya Bunduki ya Gobore wakioneshwa waandishi wa habari ( hawapo pichani)
Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano ambaye pia aliwahi kuwa Mwakilishi wa
Kiembe Samaki na Waziri katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.
Mansour Yusuf Himid akiwasili mahakamni
Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano ambaye pia aliwahi kuwa Mwakilishi wa
Kiembe Samaki na Waziri katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.
Mansour Yusuf Himid akiiongea na baadhi ya watu mbalimbali
Mansour alifikishwa mahakamani akiwa chini ya
ulinzi mkali wa polisi akisindikizwa na magari matatu huku askari wa
Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakitanda eneo zima la Mahakama wakiwa
na silaha za moto na mabomu ya machozi.
Mwendesha mashtaka, Maulid Ame Mohamed alimsomea
mashtaka matatu likiwamo la kupatikana na silaha kinyume na Kifungu 6(3)
na 34(1)(2) cha Sheria ya Silaha na Risasi namba 2 ya mwaka 1991, Sura
ya 223 ya Sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alidai kwamba Agosti 2, mwaka huu saa saba mchana
huko Chukwani, Unguja bila ya halali alipatikana na bastola aina ya
baretta yenye namba F76172W kitendo ambacho ni kinyume na sheria.
Mwanasheria huyo akisaidiwa na Raya Mselem alisema
kosa la pili ni kupatikana na risasi kinyume na Kifungu cha sita
(3)(1)(2) cha Sheria ya Risasi za moto. Mshtakiwa alidaiwa kukutwa na
risasi za moto 295 za bastola ambacho ni kinyume na sheria.
Kosa la tatu alilosomewa ni kupatikana na risasi
nyingine 112 kinyume na Kifungu cha 32(2) cha Sheria ya Silaha na Risasi
namba 2 ya mwaka 1992 ambayo inaruhusu kumiliki risasi aina hiyo mwisho
50 kwa matumizi ya silaha aina ya shortgun.
Waziri huyo wa zamani baada ya kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Khamis Ramadhan Abdallah Shaban aliyakana yote matatu.
Kabla ya kesi hiyo kuanza, Wakili Gasper Nyika
anayemtetea alitakiwa kuonyesha vibali vinavyomruhusu kufanya kazi
Zanzibar na kusababisha kesi kusimama kwa muda kabla ya hakimu kumruhusu
kuendelea baada ya kuridhishwa na kibali chake.
Hata hivyo, Hakimu Khamis alisema shtaka la kwanza
la kupatikana na silaha halina dhamana, tofauti na mashtaka ya pili na
tatu ambayo yanaruhusu mshtakiwa kupata dhamana.
Wakili Nyika anayesaidiana na Omar Said Shaban
alisema kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Zanzibar,
Kifungu cha 150 (4) namba 7 ya mwaka 2004, Mahakama Kuu ina uwezo wa
kupokea ombi la dhamana kwa kesi kama hizo kama mhusika atakuwa na
sababu za kuishawishi mahakama kumpatia dhamana.
“Tunajiandaa kuwasilisha ombi letu la dhamana
Mahakama Kuu na hilo litafanyika haraka. Bado mteja wetu ana haki ya
kupata dhamana hiyo,” alisema Wakili Nyika.
Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili
Hakimu Khamis aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 18 na mshtakiwa
kupelekwa rumande katika Gereza la Kiinua Miguu.
0 comments:
Post a Comment