Bi. Nasra Dafa (30) aliyeshambuliwa na mume wake wakati akiswali.
TUHUMA nzito ya aina yake ambayo haijawahi kutokea ambapo mkazi mmoja wa Tandale – Kwatumbo wilayani Kinondoni jijini DAR, Idd Mpenda anadaiwa kumshambulia na kumjeruhi hadi kuzimia mkewe, Nasra Dafa (30) wakati akiswali.Akizungumza na Amani huku akimwaga machozi, mwanamke huyo alisema tukio hilo lilijiri Julai 28, mwaka huu saa saba mchana wakati akiswali maeneo ya duka lake lililopo Tandale.
ILIKUWA KUSHTUKIZA
Alidai kwamba alikuwa katika kusujudu, mara mumewe alitokea na kumshambulia kwa mateke, ngumi na viatu kisha akamburuza chini hadi nje hali iliyosababisha nguo aliyovaa kuvuka na kubaki kama alivyozaliwa!“ Kama unavyoniona, nimeumia sehemu mbalimbali za mwili. Kiatu ndiyo kimeniumiza sana.
ATINGA KITUO CHA POLISI
Alisema baada ya tukio hilo kutokea alijivuta na kuvaa gauni lingine kisha akakimbilia Kituo Kidogo cha Polisi Tandale ambapo polisi walimwambia ishu yake ni nzito na kumtaka aende Kituo cha Polisi Magomeni (vyote vipo Dar).
ASIMULIA VIPIGO, UKE WENZA
Mwanamke huyo aliweka hadharani kwamba mumewe amekuwa akimpiga mara kwa mara na tatizo kubwa ni uke wenza ambapo alidai ameoa mke wa pili hivi karibuni na mapenzi baina yao yamezorota.
“Mimi kabla ya kufunga naye ndoa Januari Mosi, 2013 mume wangu alikuwa na mke mwingine lakini aliamua kumpa talaka baada ya kumweleza kuwa mimi sitaki kuwa mke mwenza.
“Tukawa tunaishi naye lakini hata hivyo hakuchukua muda mgogoro ukaanza ndani ya nyumba.
Picha hii ikionyesha majeraha ya mkononi na shingoni aliyopata Bi. Nasra Dafa.
SAKATA LAFIKA KWA NDUGU
Mwanamke huyo aliendelea kusema kwamba hali ilizidi kuwa mbaya hadi ikafika kwa wana ndugu kwa suluhu, walipatanishwa lakini baada ya muda mgogoro ukaendelea na kuna siku mumewe akamwambia ameoa mke mwingine wiki tatu nyuma.
SIKU YA TUKIO
“Siku ya tukio, nilikuwa naswali. Unajua wakati wa Mfungo wa Ramadhani lazima Muislam kuswali kwa kuzingatia taratibu zote za dini. Basi, alikuja na kuniita nitoke nje lakini sikutoka.“Niliona nimalize kwanza kuswali ndipo nitoke, lakini kabla sijamaliza akaja na kunishambulia kama niliovyokwambia kisha akachukua funguo na kufunga duka.
“Alipotoka hapo akaenda kwenye duka lingine la kuuza vocha nalo akalifunga na kuchukua fedha zote na kuondoka nazo huku muuzaji akiambiwa aende kwake,” alisema mwanamke huyo.

Amani lilifika kwenye Kituo cha Polisi Magomeni na kuambiwa na askari mmoja kuwa taarifa hizo zipo na mtuhumiwa anashikiliwa hapo, lakini akashauri atafutwe Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camilius Wambura kwa maelezo zaidi. Kamanda huyo hakupatikana ofisini kwake hadi tunakwenda mtamboni.
SHEHE MKUU ASAKWA
Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum hakupatikana kuzungumzia makosa ya mume wa Kiislamu kumpiga mkewe wakati akiswali ndani ya Mwezi Mtukufu.Hata hivyo, Maalim Hassan Yahya Hussein wa Magomeni Mwembechai alipoulizwa alisema Uislamu haujatoa ruhusa kwa mwanaume kumpiga mkewe wakati anaswali hata kama amefanya kosa kubwa kiasi gani.
“Uislamu haujaruhusu kwa hali yoyote udhalilishaji na kuna hadithi zinazokataza mtu kumdhuru mwenzake. Kuna masharti sita yamewekwa kabla ya mume kufikia hatua ya kumwadabisha mkewe,” alisema Maalim Hassan.Akaendelea: “Kabla mume hajampa adhabu mke anapaswa kwanza kumpa nasaha kwa kosa alilotenda na sharti la pili ni kumpa mawaidha ama yeye mwenyewe au atafute mtu.
“Sharti la tatu ni kumkumbusha mara kwa mara na sharti la nne ni kumhama malazi, yaani kumuacha alale peke yake. Sharti la tano, akikosa ni kwenda kushitaki kwa wazee au katika vyombo vya sheria ikiwemo kwa kadhi na viongozi wa dini.“Sita ndiyo kumpiga, lakini kipigo ambacho hakitamdhuru kwani hutakiwi kumpiga ukiwa na hasira.
0 comments:
Post a Comment