Shinji
Kagawa, Darren Fletcher na Tom Cleverley, wafungaji wanne wa penati za
United, wakishangilia ushindi wao wa penalti 5-3 dhidi ya Inter Milan.
Fletcher
akishangilia ushindi na kipa wa United David De Gea baada ya kushinda
kwa penalti na kumpa Van Gaal rekodi ya ushindi wa asilimia 100 katika
michuano hiyo.
KOCHA
Louis van Gaal ameendelea kufanya vizuri kufuatia Manchester United
kuitandika kwa penalti 5-3 Inter Milan baada ya sare ya 0-0 katika mechi
ya Kombe la Kimataifa kujiandaa na msimu mpya nchini Marekani.
Katika
mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa FedEx Field mjini Washington,
penati za Man United zilizamishwa kambani na Ashley Young, Javier
Hernandez, Tom Cleverley, Shinji Kagawa na Darren Fletcher wakati Marco
Andreolli wa Inter aligongesha mwamba.
ziara
hiyo ya Marekana imekuwa ya mafanikio kwa Van Gaal kwani ameshinda
mechi tatu mfululizo na wachezaji wake wamepata nafasi ya kumuonesha
uwezo, hivyo lawama hazitegemewi.
Kocha huyo mpya wa United anaendelea kutafuta njia ya kuutekeleza mfumo wake anaoupenda wa 3-5-2.
Kwa
mfano jana usiku, Man United walianza mchezo na washambuliaji wawili,
Wayne Rooney na Danny Welbeck. Walimaliza mchezo na Nani na Wilfried
Zaha katika nafasi hizo.
0 comments:
Post a Comment