Thursday 24 July 2014


'Nothing is done' with Di Maria - Blanc
Imechapishwa Julai 24, 2014, saa 2:38 usiku

LAURENT Blanc amegoma kuweka wazi kama Paris Saint-Germain imefanya mazungumzo juu ya kumsajili nyota wa Real Madrid, Angel Di Maria.
Di Maria alikuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Carlo Ancelotti kilichotwaa ubingwa wa UEFA msimu uliopita, lakini hatima yake ya baadaye imekuwa shakani baada ya usajili wa Toni Kroos na James Rodriguez.
Bosi wa Manchester United, Louis Van Gaal anavutiwa na mchezaji huyo mwenye miaka 26 na mashetani wakundu walifikia makubaliano binafsi mapema majira haya ya kiangazi mwaka huu.
Lakini PSG wamekuwa mstari wa mbele kutaka kumsajili nyota huyo kutokana na jeuri yao ya fedha na Rais wa klabu hiyo Nasser AL-Khelaifi aliripotiwa kufanya mazungumzo mjini Madrid.

Alipoulizwa juu ya usajili wa Di Maria, Blanc alisema; “Nawaacha mfuatilie, kwasasa hakuna chochote kilichofanyika”.

RASMI: FRANK JAMES LAMPARD ATUA NEW YORK CITY NA KUTAMBULISHWA

Karibu New York mkongwe: Lampard ametambulishwa rasmi leo na klabu ya New York City.

Imechapishwa Julai 24, 2014, saa 2:21 usiku

MAISHA ya Frank James Lampard katika klabu ya Chelsea rasmi yamefika tamati baada ya kukamilisha uhamisho wake kujiunga na New York City inayoshiriki ligi kuu soka nchini Marekani, maarufu kama MLS.
Lampard ametambuliswa rasmi leo klabuni hapo.
Kiungo huyo mwenye miaka 36 ameichezea Chelsea kwa misimu 13 na kuweka rekodi nzuri ya kuwa mfungaji bora wa kihistoria wa klabu ikiwa  ametia kambani mabao 211

Kiungo huyo anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na New York City FC majira haya ya kiangazi na wa pili mwenye jina kubwa katika ulimwengu wa soka, baada ya awali kumnasa mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania David.
New adventure: Frank Lampard was pictured at JFK Airport ahead of his unveiling at New York City FC
Maisha mapya: Frank Lampard alipigwa picha katika uwanja wa ndege wa JFK wakati akiwasili kutambulishwa na New York City FC

0 comments:

Post a Comment