Wednesday 30 July 2014

Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Ubungo, Goodluck JustineUONGOZI mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo wilaya ya kichama Ubungo unatarajiwa kujulikana Agosti 3 mwaka huu baada ya uchaguzi wa ngazi za chini katika wilaya hiyo kukamilika.

Mbali na viongozi wa wilaya hiyo kujulikana siku hiyo, pia chama hicho kimeeleza kuwa, kimejiandaa vema kuwadhibiti mamluki wasijipenyeze katika uongozi huo.

Hayo yalibainishwa na Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Ubungo, Goodluck Justine, wakati akielezea mafanikio yaliyopatikana katika uchaguzi wa ngazi za msingi, matawi na kata.

Justine alisema, ni fursa kwa kila mwanachama muadilifu wa CHADEMA Wilaya ya CHADEMA Ubungo kuwania nafasi anayoona ataimudu.

Aliongeza kuwa, katika uchaguzi wa ngazi za chini, chama hicho kimefanikiwa kujiimarisha na kuongeza wanachama zaidi.

Alisema, fomu zimeanza kutolewa jana na mwisho wa kuchukua na kurejesha itakuwa Agosti Mosi saa 10 jioni

0 comments:

Post a Comment