Wednesday, 23 July 2014

Nembo ya mashindano ya Jumuiya ya madola
Wanariadha wakijipasha misuli kabla ya kuanza kwa mashindano
Mashindano ya Jumuiya ya Madola kuanza leo mjini Glascow Scotland na kufunguliwa rasmi na Malkia Elizabeth wa Uingereza ambaye pia ni mkuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya madola.
Zaidi ya wanariadha elfu tatu wanatarajiwa kushiriki katika mashindano hayo yatakayodumu kwa muda wa majuma matatu yajayo.
Australia ndio nchi ambayo imetuma kikosi kubwa zaidi katika mashindano haya ya mwaka huu.
Takwimu rasmi zinasema kuwa Australia inaakilishwa na zaidi ya wanariadha 400.
Mataifa yote nchi wanachama wa muungano huo kutoka kanda ya Afrika Mashariki na Kati yameakilishwa kwenye mashindano ya mwaka huu.
Ushindani mkali unatarajiwa katika fani mbali mbali za michezo na macho yote ya dunia itakuwa katika shindano la riadha ambalo litatumiwa na mataifa mengi kuchagua vikosi vyao vitakavyoshiriki katika mashindano ya mabara na hatimaye kombe la dunia.
Mashindano haya yataanza rasmi hiyo kesho huku wanariadha kadhaa wa Afrika Mashariki wakijibwaga ugani kuchuana na wapinzani wao katika raundi ya kwanza ya mashindano ya Judo, Masumbwi na Table tennis.
A.I

0 comments:

Post a Comment