Usu
Millya Mwanamtandao wa Ulingo wa Katiba na wanawake ambaye alikuwa
ndiye mwezeshaji wa Mkutano huo ambao ulikuwa ni wa siku mbili
akiendelea kutoa mwongozo wa mkutano huo.
Doreen
E. Maro kutoka TAMPRODA ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba
akiwakilisha Wafugaji Akileta Mrejesho wa walichokuwa wakikijadili
katika Kundi lao juu ya mapendekezo ya kuimarisha Masuala muhimu ya
Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya
Dkt.
Macca A. Mbalwa Mkurugenzi wa Giyedo Tanzania akiwa anatoa Mrejesho
wa kile ambacho walikuwa wamekijadili na kutoa mapendekezo yao ya
Kuboresha masuala muhimu katika Rasimu ya pili ya Katiba Mpya.
Salama
Aboud Talib Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Naibu Katibu Mkuu wa
UWT akizungumzia makosa mbalimbali ambayo yapo katika Rasimu ya Pili ya
Katiba mpya na kutoa mapendekezo kuwa Iboreshwe ili kuweka usawa.
Executive
Director wa Women Fund Tanzania Mary Rusimbi akizungumza juu ya
Majumuisho ya pomoja na Kupanga mikakati ambayo yatasaidia Kuimarisha
Masuala Muhimu ya Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya
Mgeni
Hassan Juma Mwenyekiti wa Wawakilishi Wanawake Zanzibar akitoa neno la
Shukurani kwa wote waliohudhuria kwa muda wa siku mbili katika mkutano
wa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mtandao wa wanawake na TAMWA
Profesa Ruth Meena Akitoa Majumuisho pia kutoa Shukurani kwa wale wote waliohudhuria katika Mkutano huo uliochukua siku mbili.
Valerie Msoka akifunga Rasmi Mkutano huo.
Fredrick
Msigala Mjumbe Bunge Maalum la Katiba ambaye ni Mlemavu wa Miguu
akielezea masikitiko yake ya Jinsi watu wenye ulemavu wakiwemo wanawake
na wanaume ambavyo wametengwa na kukosa haki zao, amesisitiza Serikali
katika Rasimu Mpya ya Pili ya Katiba wawaangalie walemavu kwa umakini na
ukaribu maana wanahaki sawa na watu wengine. Pia amesisitiza walemavu
wajaliwe katika huduma za Afya mana ni Muhimu kwao. Mwisho amesisitiza
kuwa wanawake wenye ulemavu wanahaki ya Kuolewa na kuto nyanyaswa pindi
wanapokuwa katika ndoa zao.
Modesta
Mpereme ambaye ni Kiziwi hasikii lakini anaongea vizuri pia ni
Mwenyekiti kutoka Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania, Ameiomba
serikali iwe na vitendea kazi vya kutosha ambavyo vitawasaidia walemavu
katika secta mbalimbali Mfano katika Mabenki kuwe na vifaa maalum vya
kuwasaidia walemavu, Katika Upande wa Afya amesisitiza kuwe na hata watu
wanaoweza kutoa msaada wa kutafsiri mambo mbalimbali mfano kwa Viziwi,
wasio ona na ambao Hawawezi kuongea.
Siti
Ally Mwanasheria na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba kutoka Zanzibar
akisisitiza umuhimu wa usawa kati ya haki za wanawake na wanaume katika
jamii , Pia alisisitiza juu ya mabinti wanaopata Mimba za utotoni wakiwa
mashuleni na kusisitiza kuwa wanaruhusiwa kusimama masomo mpaka kipindi
mtoto atakapokuwa mkubwa anaruhusiwa kuendelea na masomo, Mwanaume
aliyesababisha Mimba anaweza akashtakiwa .
Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la katiba pamoja na Wadau mbalimbali waliofika katika Mkutano huo.
0 comments:
Post a Comment