Wednesday 23 July 2014

Muindaji haramu ahukumiwa miaka 77 jela

 23 Julai, 2014 - Saa 17:34 GMT
Pembe ya Faru yasabisha afungwe miaka 77 jela
Mtuhumiwa wa uwindaji haramu Mandla Chauke amehukumiwa kifungo cha miaka 77 jela kwa kuwauwa vifaru 3 mwaka wa 2011 nchini Afrika Kusini.
Hiyo ndiyo hukumu kali zaidi kuwahi kutolewa katika jitihada za kukomesha uwindaji haramu nchini humo.
Chauke anatuhumiwa kwa kuwaua vifaru 3 katika mbuga ya wanyama ya Kruger National Park .
Wawindaji haramu waliua takriban vifaru 1,004 mwaka uliyopita na kuzua hofu huenda wanyama hao wa porini wakaangamia iwapo hawatalindwa na kuhifadhiwa.
Afrika Kusini ni mwenyeji wa asilimia 70% ya vifaru wote duniani.
Habari za kifungo hicho cha kihistoria zilieneo kote nchini Afrika Kusini na kufurahiwa na wanaharakati wa uhifadhi wanyama wa porini .
Pembe ya Faru yasabisha afungwe miaka 77 jela
Mahakama hiyo vilevile ilimhukumu Chauke kwa kusababisha kifo cha mshirika wake wa karibu aliyepigwa risasi na askari wa kulinda wanyama .
Mwaka wa 2012 mahakama moja nchini humo ilimhukumu raiya mmoja wa Thailand kifungo cha miaka 40 gerezani kwa kosa la kuuza pembe za vifaru.
Pembe ya kifaru inayouzwa katika soko la magendo inagharimu takriban dola elfu $95,000 kwa kilo bei ambayo inaiweka juu ya dhahabu duniani.
Duru zinaashiria kuwepo kwa genge la wawindaji haramu ambao wanaua na kuuza pembe za vifaru katika Mashariki ya kati na Mashariki ya mbali.
Huko Asia pembe za ndovu zinadhaminiwa kuwa ishara ya ukwasi mbali na kuwa na uwezo wa kuongeza nguvu za kiume

0 comments:

Post a Comment