Thursday, 31 July 2014

Taarifa ya jeshi la polisi mkoa wa mbeya kwa vyombo vya habari “press release” tarehe 31.07.2014.

    Watu wanne wafariki dunia na wengine 51 kujeruhiwa katika ajali ya gari matundasi wilayani chunya.

    Mtu mmoja afariki dunia katika ajali ya barabarani jijini mbeya.

    Mtoto wa miaka mitatu afariki dunia baada ya kuangukiwa na kifusi cha mchanga wilayani chunya.

    Mtoto wa miaka kumi afariki dunia baada ya kupigwa na shoti ya umeme.

Katika tukio la kwanza:
 Watu wanne waliotambulika kwa majina ya 1. paulo mwasanga (18) mkazi wa kitongoji cha matundasi ‘b’ 2. wedi angolwise (21) mkazi wa matundasi 3. salome mwakibete (13) mwanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi sambilimwaya na 4. obedi mwakamela (25) mkazi wa matundasi wamefariki dunia papo hapo baada ya gari lenye namba za usajili t.595 chu aina ya fuso tipper likiendeshwa na dereva asiyefahamika jina kipinduka katika kijiji cha matundasi wilayani chunya.
Ajali hiyo ilitokea mnamo tarehe 30.07.2014 majira ya saa 16:00 jioni huko katika kitongoji cha matundasi “b”, kijiji cha matundasi, kata ya matundasi, tarafa ya kiwanja, wilaya ya chunya, mkoa wa mbeya katika barabara ya chunya/makongolosi.

 gari hilo lilikuwa likitokea kijiji cha sambilimwaya kuelekea kijiji cha matundasi likiwa limebeba wachezaji wa mpira wa miguu na mashabiki. aidha katika ajali hiyo watu 51 walijeruhiwa, kati yao 26 walitibiwa na kuruhusiwa na wengine 25 wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya chunya wakiendelea kupatiwa matibabu. chanzo cha ajali ni mwendo kasi, dereva alikimbia mara baada ya tukio na juhudi za kumtafuta zinaendelea.
 kaimu kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi wa polisi barakael .n. masaki anatoa wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto hasa kwa kuzingatia sheria na alama za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika. aidha anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za mahali alipo mtuhumiwa azitoe katika mamlaka husika ili akamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

 katika tukio la pili:
 mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la wile peter ambaye alikuwa abiria katika pikipikiamefariki dunia baada ya gari lenye namba za usajili dfp 0036 aina ya benz mali ya shirika la umeme tanesco lililokuwa  likiendeshwa na patrick mhagama (46) mkazi wa ilomba jiji mbeya kumgonga mpanda pikipiki asiyefahamika jina wala makazi yake na kusababisha kifo kwa abiria huyo.

 Ajali hiyo imetokea mnamo tarehe 31.07.2014 majira ya saa 16:45 jioni huko nzovwe, kata ya nzovwe, tarafa ya iyunga, jiji na mkoa wa mbeya. chanzo cha ajali kinachunguzwa. dereva amekamatwa na gari lipo kituoni. mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa mbeya.
 Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi wa polisi barakael .n. masaki anatoa wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto hasa kwa kuzingatia sheria na alama za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.

 Katika tukio la tatu:
 Mtoto mwenye umri wa miaka mitatu aliyetambulika kwa jina la pascalia jifula ngasa amefariki dunia baada ya kuangukiwa na kufunikwa na kifusi cha mchanga katika kitongoji cha chizya wilayani chunya.

 Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 30.07.2014 majira ya saa 08:300 asubuhi huko katika kitongoji cha chizya, kijiji cha mwambani chini, kata ya mwambani, tarafa ya kwimba, wilaya ya chunya, mkoa wa mbeya. wakati tukio hilo linatokea, mtoto huyo alikuwa akicheza na watoto wenzake kwenye gema la mchanga na ndipo kifusi kumuangukia na kumfunika.

 Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi wa polisi barakael .n. masaki anatoa wito kwa wazazi na walezi kuwa makini na watoto wadogo kwa kuangalia mazingira ya maeneo yao ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.

 katika tukio la nne:
 Mtoto wa miaka kumi aliyefahamika kwa jina la jerry jested, mwanafunzi na mkazi wa mlowo wilayani mbozi alikutwa amekufa chumbani kwake baada ya kupigwa na shoti ya umeme.

 Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 30.07.2014 majira ya saa 06:00 asubuhi huko katika kata ya mlowo, tarafa ya vwawa, wilaya ya mbozi, mkoa wa mbeya. inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni baada ya marehemu kulamba nyaya za umeme ambazo zilikuwa karibu na kitanda chake hali iliyopelekea kupigwa shoti na kusababisha kifo chake.

 Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi wa polisi barakael .n. masaki anatoa wito kwa wazazi na walezi kuwa makini na watoto wadogo kwa kuangalia mazingira ya maeneo yao ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza ikiwa ni pamoja na kuweka mbali vitu vya hatari kwa watoto.
 imetolewa na kusainiwa na:
 [barakael .n. masaki – acp]
kaimu kamanda wa polisi mkoa wa mbeya.

0 comments:

Post a Comment