Thursday 24 July 2014

TAIFA1
WANANDINGA wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars wana matumaini ya kuwafunga Msumbiji (Black Mambas) katika mechi ya marudiano itakayopigwa kati ya Agosti 2 na 3 mwaka huu kwenye uwanja wa taifa wa Zimpeto mjini Maputo.
Taifa stars ilitoka sare ya mabao 2-2 mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya Mambas ndani ya dimba la Taifa jijini Dar es salaam, hivyo wanahitaji ushindi wa mabao 1-0 au sare ya mabao 3-3 ili kufuzu hatua ya makundi kusaka tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya Africa, AFCON, nchini Morocco.
Mlinda mlango namba mbili wa Stars ambaye katika mechi iliyopita alikaa benchi, Aishi Manula amesema kama  Msumbiji walipata  mabao mawili Dar es salaam nao wanaweza kupata ushindi mjini Maputo.(A.I).

0 comments:

Post a Comment