Monday 28 July 2014

Wasamalia wema wakijaribu kulinasua gari aina ya Toyota Corolla (namba zake za  usajili hazikuweza fahamamika mara moja kutokana na kutokuwepo)  lililoingia kwenye mtaro baada ya dereva wake kuzidiwa maarifa ya  kiudereva na kujikuta akiingia mtaroni,katika eneo la Mafiat mkabala na  kituo cha mafuta cha Oilcom jijini Mbeya asubuhi hii.

Dereva wa Gari hilo pamoja na mtu mwingine mmoja wamejeruhiwa na kukimbizwa hospital kwa  matibabu.Chanzo cha ajali hiyo inaelezwa ni mwendo kasi aliokuwa nao  Dereva wa gari hilo.
Wasamalia wema hao wakiangalia namna ya kuweza kulichomoa gari hilo.
Hayaaaa..... Moja.... mbili.... tatuuu twendeeeeeeee......
Mara wakafanikiwa kulitoma kwenye mtaro huo.Picha na Fadhil Atick,Mbeya

0 comments:

Post a Comment