Saturday, 19 July 2014



JAMES-RODRIGUEZ-BESTKWA mujibu wa habari toka Gazeti la 'Le Parisien' huko France, AS Monaco inadai ilipwe Euro Milioni 85 kutoka Real Madrid kwa ajili ya Uhamisho wa Straika James Rodriguez. Rodriguez, Staa wa Colombia mwenye Miaka 23, alipanda chati mno huko Brazil alipong’ara na Colombia na kuweza kuibuka kuwa Mfungaji Bora wa Fainali za Kombe la Dunia na kutwaa Buti ya Dhahabu. Ripoti hizi za Leo pia zinadai Rodriguez tayari ashaafikiana na Real kuhusu maslahi yake binafsi na atalipwa Euro Milioni 8 kila Msimu kwa Mkataba wa Miaka Mitano. Hivi sasa Rodriguez, ambae alitokea FC Porto Mwaka 2013 kwa Dau la Euro Milioni 45, ana Mkataba na AS Monaco hadi 2018. Lakini inaaminika huenda Real ikalishusha Dau hilo wanalotaka AS Monaco kwa kulipa Fedha kidogo na kuwapa Mchezaji mmoja juu ili ahamie huko France. Supercopa de España
Real Madrid na Atlético Madrid zimefikia makubaliano na Wasimamizi wa La Liga, LFP, [Professional Football League] kusogeza Ratiba zao za Ligi ili kupisha Mechi zao mbili za Supercopa de España.
Supercopa de España hushindaniwa kati ya Bingwa wa La Liga na Mshindi wa Copa del Rey. Timu hizo zinapaswa kukutana kwenye Kombe hilo kwa sababu Atletico ndie Bingwa wa La Liga na Real wao ndio waliobeba Copa del Rey Msimu uliopita. Kufuatia kukubaliana na LFP kusogeza Mechi zao za La Liga kuchezwa Jumatatu Agosti 25, Mechi za Supercopa de España sasa zitachezwa Jumanne Agosti 19 huko Santiago Bernabeu na kurudiana Ijumaa Agosti 22 huko Vicente Calderon. Mara ya mwisho kwa Timu hizi kutwaa Supercopa de España ni 2012 kwa Real Madrid kuibwaga Barcelona [2-3 na 2-1] na 1985 kwa Atletico Madrid walipoilaza Barcelona [3-1 na 0-1]. Barcelona ndio wametwaa Kombe hili mara nyingi, mara 11, wakifuatiwa na Real Madrid, mara 9, Deportivo La Coruna mara 3 na Atletico Madrid mara 1.

0 comments:

Post a Comment